Customer Feedback Centre

Ministry of Health

RAIS SAMIA ATOA BILIONI 49 KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA NJOMBE

Posted on: October 26th, 2023

Na. WAF - Njombe 


Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewekeza kiasi cha shilingi Billioni 49 katika kuboresha huduma za afya katika mkoa wa Njombe katika kipindi cha mwaka 2023. 



Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel Mkoani Njombe wakati akisalimia wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe na watumishi wa kiwanda cha Mbao cha TAN wakati wa ziara ya Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango mkoani Njombe.


Dkt. Mollel ameeleza kuwa fedha hizo zimeleta mabadiliko makubwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe ikiwemo kufanya Maboresho na kuwezesha upatikanaji wa Dawa, vitendanishi, Vifaa tiba vya Kisasa, matibabu ya kibingwa na bingwa bobezi pamoja na wataalam zaidi.


Aidha, amesema kutokana na Ujenzi wa Kiwanda cha kutengeneza mipira ya Mikono (Gloves) Tanzania inatarajia kupata faida ya uzalishaji kwa asilimia 83.4 ikiwa ni mahitaji ya Nchi nzima.