Customer Feedback Centre

Ministry of Health

RAIS DKT. SAMIA AFIKISHA HUDUMA ZA KIBINGWA NA UBINGWA BOBEZI KWA AFYA YA MSINGI.

Posted on: May 6th, 2024



Na WAF - RUVUMA

Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Tamisemi imezidi kusogeza huduma za kibingwa na Ubingwa bobezi kwa njia ya Mkoba hadi katika Afya ya Msingi kupitia Madaktari bingwa wa Rais Dkt. Samia kwa hospitali za halmashauri 184 toka Mikoa 26 nchini ikiwemo hospitali za Halmashauri 8 za Mkoa wa Ruvuma.

Hilo limebainika leo Mei 6, 2024, Wilayani Songea Mkoani Ruvuma wakati wa uzinduzi wa Mpango kabambe wa Madaktari bingwa wa Dkt. Samia kwa Halmashauri 184 wenye kauli mbiu "TUMEKUFIKIA, KARIBU TUKUHUDUMIE" uliozinduliwa na Kaimu Katibu Tawala Mkoa (Miundombinu )Mhandisi Gilbert Simiya ambaye amemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas


"Naipongeza Serikali kwa kuja na utaratibu wa Madaktari bingwa wa Dkt. Samia ambapo leo tunashuhudia madaktari bingwa wa huduma za kibingwa Bobezi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Kanda yetu ya Nyanda za juu kusini ambapo Huduma za Matibabu ya kibingwa na Ubingwa Bobezi kwa Mkoa wa Ruvuma kwa kutumia Madaktari bingwa kwenda kuwajengea uwezo wataalam wa hospitali za Halmashauri 8 "amesema Mhandisi Simiya.

Amesema huduma za Kibingwa zitakazo tolewa ni huduma za uzazi, wajawazito na magonjwa ya wanawake, Huduma za afya kwa watoto na watoto wachanga, Huduma za upasuaji na mfumo wa mkojo, Huduma za usingizi na ganzi, Huduma za Daktari bingwa magonjwa ya ndani, magonjwa ya akina mama na uzazi, Magonjwa ya ndani kama vile shinikizo la damu, kisukari, figo na Magonjwa ya Watoto.

Kwa upande wake Mratibu wa huduma za Afya ya Uzazi kutoka wizara ya Afya Bi Faraja Mgeni amesema Lengo ni kufikisha huduma za kibingwa na bobezi kwenye hospitali 184 ngazi ya halmashauri katika Mikoa yote 26 ya Tanzania Bara.