MPANGO JUMUISHI WA HUDUMA ZA AFYA NGAZI YA JAMII MSINGI WA AFYA BORA, LISHE, USTAWI WA JAMII
Posted on: September 27th, 2025
Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma kutoka Wizara ya Afya Dkt. Ona Machangu amesema Mpango Jumuishi wa Hudumu wa Afya Ngazi ya Jamii una umuhimu mkubwa katika msingi wa afya bora, lishe na ustawi wa jamii.
Dkt. Machangu amesema hayo Septemba 25, 2025 mkoani Ruvuma ikiwa ni mwendelezo wa timu ya wataalam wa afya kutoka Wizara ya Afya na Ofisi ya Rais TAMISEMI kufanya Usimamizi Shirikishi wa utekelezaji wa Mpango Jumuishi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii .
"Mpango Jumuishi wa Wahudumu wa Afya Ngazi za Jamii una umuhimu mkubwa katika kuimarisha afya bora, lishe na ustawi wa jamii, hivyo sote tuna wajibu katika kuhakikisha tunasimamia ipasavyo," amesema Dkt. Machangu.