Customer Feedback Centre

Ministry of Health

MADAKTARI BINGWA WA RAIS SAMIA WAVUNJA REKODI, WAHUDUMIA WANANCHI 800 KWA SIKU.

Posted on: May 6th, 2024



Na. WAF - MOROGORO.

Wananchi zaidi ya 800 wamepata huduma za matibabu bingwa kupitia Madaktari bingwa na ubingwa bobezi wa Rais Samia kanda ya kati iliyoweka kambi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro ikiwa ni siku ya kwanza ya Kambi hiyo.

Hayo yamesema na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro Dkt. Daniel Nkungu leo tarehe Mei 6, 2024 Mkoani Morogoro wakati akitoa tathimi ya siku juu ya utoaji wa huduma hiyo.

Dkt. Nkungu amesema muitikio wa wananchi ni mkubwa na kuongeza kuwa kambi hiyo imeweza kufanya pasuaji kumi na mbili kwa siku ya kwanza na kumshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Waziri ya Afya Mhe. Ummy Mwalimu kwa uboreshaji na utekelezaji wa kambi za matibabu ya madaktari bingwa na ubingwa bobezi kwa wananchi ambayo inaleta unafuu mkubwa wa matibabu kwa watanzania.

“Tunashukuru wananchi wa maeneo yote wameweza kuja kwa wingi kupata huduma tunazozitoa , watu walifika zaidi ya 1000 lakini kulingana na muda tumeweza kuona wananchi 800, Tunamshukuru Mkuu wa wilaya ya Kilosa kwa kutoa gari na kuleta wananchi kuja kupatiwa matibabu katika kambi hii “ Amesema Dkt. Nkungu.

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa magonjwa ya Sikio, Pua na Koo Dkt. Costantine Kaniki ametoa rai kwa wananchi kuacha tabia ya kujisafisha kiholela masikio yao na kuwataka kufika hospitali pale wanapota maumivu ( vox pop) na kuongeza kuwa watu wajitokeze kwa wingi kwenye kambi hiyo ili kujua Afya zao.

“Leo tumeweza kuwahudumia wananchi zaidi ya 200, wananchi wengi wanoakuja hapa ni wale wanaotumia njia holela kujisafisa masikio kwa kuingiza pamba na kadhalika, na pia nitoe rai kwa wananchi kuacha tabia ya kutumia kila aina ya dawa wanapopata shida ya masikio bila kufika katika kituo cha kutolea huduma za afya” . Ameeleza Dkt. Kaniki.

Bi. Hidaya Masenye, Mkazi wa Kata ya Mkundi Mkoa wa Morogoro amefurahia huduma za Madikatari bingwa hao kwa kupatiwa huduma kwa uharaka na kuiomba serikali kuendelea kuiwezesha huduma hiyo mara kwa mara pamoja na kumshukuru Rais Dkt. Samia kwa kuileta karibu na wananchi huduma ya kambi ya matibabu ya Madaktari bingwa na Ubingwa Bobezi.