MADAKTARI BINGWA WA RAIS SAMIA MTUACHIE ALAMA WANADODOMA
Posted on: September 23rd, 2024Na WAF-DODOMA
Jumla ya Madaktari Bingwa na Bingwa Bobezi wa Rais Samia wapatao 50 wamepokelewa mkoani Dodoma na Mkuu wa mkoa Mhe. Rosemary Senyamule na kuwataka kwenda kuwahudumia watanzania wa mkoa huo kwa siku zote sita watakazokuwepo kwenye Halmashauri zote nane za mkoa huo kwa moyo wa Upendo na kuacha kumbukkumbu hata wakiondoka.
Mhe. Senyemule ameyasema hayo Septemba 23, 2024 wakati wa mapokezi ya Madaktari watakaofanya kazi za Kibingwa na Bingwa Bobezi sambamba na kuwajengea uwezo watumishi wa Afya waliopo kwenye ngazi za msingi.
“Tunataka mtakapo ondoka muacha alama kwa wananchi lakini pia watumishi ambao kwa namna moja au nyingine mtakuwa mkishirikiana nao bega kwa bega muda wote na kuwajengea uwezo mkoani kwetu kwenye Halmashauri zote nane” amesisitiza Senyamule.
Mhe. Senyemule amesema wanafarijika kuona uwekezaji mkubwa uliofanya na Serikali upande wa miundombinu ya afya na sasa wanapelekewa Madaktari Bingwa na Bobezi kwa ajili yakutatua changamoto za afya kwa wananchi wa ngazi ya msingi.
“Zamani Madaktari Bingwa ungeweza kukutana nao kwenye Hospitali maalum hasa zile zilizojulikana kama za Kanda lakini pia taifa lakini leo, Mabingwa ninyi mnashuka hadi kwenye ngazi ya Halmashauri kwa ajili yakushughulikia afya za watanzania, kipekee nimshukuru sana Rais Samia kwa maono yake ya kujali na kuwasogezea wananchi Huduma za afya karibu,” ameongeza Mhe. Senyamule
Akitoa salama za wizara Dkt. Mathew Mushi kutoka Wizara ya Afya ameeleza kuwa malengo ya zoezi hilo ni muendelezo wa kambi ya awamu ya kwanza iliyofanyika kwa mafanikio ambapo wananchi zaidi ya 70,000 waalifikiwa na Huduma hizo za ubingwa na bingwa bobezi.
“Katika awamu hii shabaha nikuwafikia wananchi 100,000 kwa huduma zote tutakazozitoa kwenye Halmashauri 184 kote nchini” amesema Dkt. Mushi”, na kuongeza