Customer Feedback Centre

Ministry of Health

HUDUMA ZA KINGA, TIBA, ELIMU YA AFYA KUPEWA KIPAUMBELE KITITA CHA TAIFA CHA AFUA MUHIMU ZA AFYA

Posted on: October 22nd, 2024

Na WAF- Dar es Salaam,

Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Tumaini Nagu ametoa angalizo kwa wadau wa sekta ya afya kuhakikisha kuwa huduma za afya zinazopendekezwa kupewa kipaumbele zinajumuisha huduma za elimu ya afya kwa umma, kinga, tiba na urekebishaji.

Prof Nagu ameyasema hayo leo tarehe 22 Oktoba, 2024 jijini Dar es Salaam, katika kikao kazi kinachoandaa kitita cha Taifa cha afua muhimu za afya.

Prof. Nagu amesema Serikali imeweka uwekezaji mkubwa katika huduma za afya, ikiwemo kuboresha miundombinu ya kutolea huduma za afya hivyo ni mipango ya Serikali kwamba kila mwananchi apate huduma za afya anazohitaji, pale alipo bila ya vikwazo vyovyote. Vikwazo hivi vinaweza kuwa vya kijiografia na vya kifedha.

"Huduma za afya zinazopewa vipaumbele zinaweza zikatofautiana kati ya nchi na nchi kutegemeana na uwezo wa kifedha, tuzingatie katika kazi hii gharama ya kitika hiki ifanyike kwa umakini, kila mmoja ahakikishe amatumia ujuzi wake ipasavyo ili kuhakiisha kitita hiki kitatekelezeka katika mfumo wetu wa afya," amesema Prof. Nagu.

Pia Prof. Nagu amesisitiza kuhakikisha maoni ya watumiaji wa huduma za afya yanatiliwa yanazingatiwa, sambamba na kuangalia visababishi vya vifo vinavyotokea katika jamii.
Nagu.