Customer Feedback Centre

Ministry of Health

FANYENI TAFITI ILI KUBORESHA HUDUMA ZA MAABARA

Posted on: November 29th, 2023

Na: WAF, Dodoma


Wahititimu wa mafunzo ya uongozi wa maabara chini ya programu ya Global laboratory Leadership Program (GLLP) wametakiwa kufanya tafiti katika huduma za uchunguzi wa magonjwa katika sehemu ya usimamizi wa huduma za maabara ili kudumisha huduma za uhakika katika maabara Nchini.


Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Huduma za Dharura na maafa Wizara ya Afya Dkt. Elias Kwesi wakati akimuwakilisha Katibu mkuu wa Wizara ya afya Dkt. John Jingu katika mahafali ya mafunzo ya uongozi wa maabara kupitia programu ya Global Laboratory Leadership Program iliyofanyika Novemba 29, 2023 jijini Dodoma.


Dkt. Kwesi amesema kupitia tafiti ambazo zitafanywa na wahitimu haoz itasaidia katika kuchunguza na kugundua namna ya kuboresha huduma za maabara katika hospitali, vituo vya afya na zahanati.


“Nendeni mkafanye tafiti, tafiti hizi zitasaidia katika kuboresha huduma za maabara hasa katika uchunguzi wa magonjwa na kuboresha huduma zenyewe”. Amesema Dkt. Elias.


Aidha Dkt. Kwesi amesema ili kuweza kufanikiwa ni vyema kwa wahitimu wakazingatia na kuyafanyia kazi mafunzo waliopata ili kudumisha ubora Nyanja za maabara kwa kutoa huduma nzuri..


Hata hivyo Dkt. Kwesi ameongeza kuwa eneo la maabara ni eneo la heshima, hivyo ukiingia maabara unatakiwa uwe na heshima kwai ni sehemu nyeti kwa ajili ya uchunguzi na utoaji wa huduma.