DKT. KIKWETE KUENDELEA KUTOA MCHANGO HUDUMA ZA UZAZi, MAMA NA MTOTO
Posted on: January 24th, 2023
Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amesema huduma za Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto ni suala ambalo lipo ndani ya moyo wake na ataendelea kutoa mchango kwa Serikali na wananchi kwa ujumla.
Dkt. Kikwete ameyasema hayo wakati alipotembelewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi kwenye ofisini kwake jijini Dar ea Salaam.
Dkt. Kikwe amesema anaishukuru Serikali kupitia Wizara ya afya kwa kuendelea kumwamini na kumtumia katika mchango wake wa kuboreaha huduma katika sekta ya afya nchini.
Naye, Katibu Mkuu,Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi ametoa shukrani kwa Mhe. Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Kiwete kwa mchango wake mkubwa katika sekta ya Afya alipokiwa Rais na baada ya kustaafu hususan katika eneo la afya ya msingi, rasilimali watu, mafunzo ya kibingwa, afya ya mama na mtoto, huduma za meno na uwekezaji mkubwa katika Hospitali ya JKCI, Mlonganzila, Benjamin Mkapa na Chuo kikuu cha CUHAS.
Aidha, hadi sasa Rais Mstaafu anaendelea kutoa ushirikiano yeye binafsi na taasisi yake ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation kwa Wizara ya afya katika jitihada za kuboresha huduma za afya hususani huduma za Uzazi, Mama na Mtoto na ameendelea kuwa Balozi wa jitihada za kuboresha sekta ya afya.