Customer Feedback Centre

Ministry of Health

DAKTARI, MGONJWA KWENDA KIDIJITALI, KUWASILIANA KABLA YAKUFIKA ENEO LA HUDUMA

Posted on: May 16th, 2024



Na WAF - Dar es Salaam

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. John Jingu, amesema Serikaki kupitia Wizara ya Afya iko mbioni kuanzisha mfumo wa kuweka ahadi baina ya Watoa huduma.z Afya na Wapewa huduma ili kuwapnguzia wagonjwa adha ya kukaa muda Mrefu wakisubiri huduma.

Dkt.Jingu ameyasema hayo Leo Mei 16 Jijini Dar Es Salaam wakati siku ya pili ya Ziara yake ya kukagua Miradi ya ujenzi inayoendelea katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Amana,

Amesema Serikali imeona ipo haja ya kuja na mfumo huo ikiwa ni jitihada za kutumia Teknolojia kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma za Afya.

"Nimelisisitiza hapa ni kuwa na mfumo wa Miadi Hospitalini, kwamba popote unapokuwa unafanya miadi na kupunguza upotezaji wa muda unaposubiri huduma kituoni au Hospitalini, Hospitali, ni lazima kutatumia huo mfumo kuboresha hali ya utowaji wa huduma na watu kuacha kuamka usiku wa manane kwenda kwa muda aliopangiwa huku akiwa hana uhakika wa Huduma" amesema Dkt. Jingu

Dkt Jingu ameongeza kuwa Kabla ya kuanza matumizi Rasmi ya Mfumo huo Serikali kupitia wizara ya Afya itahakikisha na inatoa elimu sahihi ya Matumizi ya Mfumo huo kwa wananchi wote ili kila kada iweze kunufaika na Teknolojia hiyo.

Katika hatua nyingine Dkt. Jingu amekabidhi Hati ya umiliki wa eneo la Hospitali ya Rufaa ya Amana kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Bryceson Kiwelu, baada ya kukaa muda mrefu bila hati ya umiliki wa eneo hilo.

" Hati hii inatuonyesha tuna eneo hapa Takribani hekari 6.3 nimekukabidhi ili ikusaidie kwenye Mipango kwakuwa utakuwa unajua eneo ulilonalo" amesema Dkt Jingu

MWISHO