Wizara Ya Afya

SHIMIWI 2026: WIZARA YA AFYA YANG'ARA MCHEZO WA RIADHA

Posted on: October 4th, 2026

Na Zakayo Mosha, WAF- Kilimanjaro

Timu ya Mchezo wa Riadha kutoka Wizara ya Afya imefanya vizuri kwa wanariadha wa timu hiyo kupata medali kwa kushika nafasi za juu na kuendelea kuwa tishio katika mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali(SHIMIWI) yanayoendelea mkoani Kilimanjro.

Akizungumza leo oktoba 3,2026 mkoani Kilimanjaro Bw.Festo Mgata Mwenyekiti wa Michezo Wizara ya Afya baada ya kukamilika hatua ya fainali ya mchezo wa Riadha, amesema mkimbiaji Philbert Baitu ameshika nafasi ya pili katika mbio za mita 200 wanaume.

Amesema, katika mbio za mita 1,500 mkimbiaji wetu *Joseph Kachala* ameshika nafasi ya pili na kuchukua medali, ameeleza kuwa katika mbio za mita 3000 pia Joseph Kachala tena ameshika nafasi ya tatu na kutunukiwa medali.

"Wanariadha wa Wizara ya Afya pia walifanikiwa kuingia fainali katika mchezo wa kukimbia na vijiti mita 800 na mita 100 wanaume ambapo walionesha ushindani mkubwa katika mashindano hayo mwaka 2026" amesema na kuongeza Bw.Festo.