Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

SERIKALI KUKAMILISHA UJENZI WA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA SONGWE KWA WAKATI

Posted on: November 23rd, 2023



Serikali kupitia Wizara ya Afya imepanga kukamilisha ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe iliyopo katika kata ya Vwawa, Wilaya ya Mbozi mkoani humo kabla ya mwaka 2025

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na wanachi Hospitalini hapo leo katika ziara yake ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Hospitali hiyo

Mhe. Majaliwa amesema Rais wetu Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan ataendelea kuleta fedha za kutosha mkoani Songwe ili kuhakikisha ujenzi wa Hospitali hiyo unakilika kwa wakati

"Ujenzi unaendelea na mpaka sasa Serikali imetumia shilingi bilioni 13 katika ujenzi wa majengo yaliyopo hapa na tunatarajiwa kutumia shilingi Bilioni 37 mpaka kukamilika kwake". Amesema

Pia Mhe. Majaliwa amesema kukamilika kwa ujenzi wa Hospitali hiyo ita imarisha huduma za Tiba utalii nchini kwa kuhudumia wagonjwa mbalimbali kutoka nchi za jirani

"Hospitali hii inayojengwa hapa Songwe ni ya kimkakati, mkoa huu unapakana na nchi za jirani za zambia na malawi ndugu zetu kwahiyo ndugu zetu wa jirani wa karibu watakuwa wakina hapa mbozi kutibiwa". Amesema

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel amesema vifaa Tiba muhimu vyote vya kuweka katika Hospitali hyo vipo tayari kwa kufungwa ikiwemo kifaa cha CT Scan ambacho ndani ya siku 21 kitakuwa tayari kimeshafungwa Hospitalini hapo.

"Ndani ya hospitali hii kuna majengo yanamaliziwa lakini vifaa tiba vyote vipo hapa na vingine vipo kanda kwa ajili ya kuweka kwenye majengo ambayo yamemalizika, watu watakuwa hawana haja ya kusafiri zaidi ya kilometa 100 kwenda mbeya kufuata huduma za vifaa hivyo". Amesema Dkt. Mollel