MABALOZI ELIMU YA MAAFA NA DHARURA, MGUU SAWA KUKABILI MAJANGA NGAZI YA MSINGI
Posted on: March 15th, 2026Na Andrea Kadege, WAF-Korogwe
Timu za Haraka za Kukabiliana na Dharura (Rapid Response Team-RRTr) kuwa mabalozi wa kufikisha elimu kuhusu maafa na dharura za kiafya katika ngazi ya jamii ili kusaidia wananchi kuelewa namna bora ya kujikinga na kukabiliana na matukio ya mlipuko wa magonjwa na majanga mengine.
Hayo yamebainishwa Mganga Mkuu wa mkoa wa Tanga, Dkt. Japhet Simeo wakati akifunga mafunzovya RRT huku akisisitiza kuwa washiriki wa mafunzo hayo wanapaswa kutumia ujuzi walioupata kuwaelimisha wataalam wengine na wananchi katika ngazi ya msingi ili kuongeza uelewa wa jamii kuhusu hatua za awali za kukabiliana na dharura za kiafya.
Dkt. Simeo amesema mafunzo hayo ni muhimu kwa kuimarisha uwezo wa wataalamu wa afya kukabiliana kwa haraka na matukio ya dharura, hivyo akasisitiza kuwa yanapaswa kuwa endelevu na yenye tija ili kuhakikisha timu hizo zinakuwa tayari wakati wote kukabiliana na changamoto za kiafya zinapotokea.
Aidha, amewataka washiriki wa RRT kuzingatia umuhimu wa kuelewa utamaduni na mazingira ya jamii wanazokwenda kutoa huduma, akieleza kuwa uelewa huo husaidia kutoa huduma kwa ufanisi na kujenga ushirikiano mzuri kati ya watoa huduma na wananchi.
Kwa upande Mratibu-Udhibiti Maafa na Dharura kutoka Wizara ya Afya Dkt. Saumu Nungu, amesisitiza dhamira thabiti ya Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo kuimarisha mifumo ya kinga, utayari na mwitikio katika kukabiliana na majanga na dharura za kiafya huku juhudi hizo zinalenga kuhakikisha jamii inalindwa dhidi ya athari za matukio ya dharura kwa kuimarisha uwezo wa wataalamu wa afya pamoja na mifumo ya utoaji huduma katika ngazi mbalimbali.
Aidha, amezipongeza Timu za Haraka za Kukabiliana na Dharura (RRT) za Mkoa wa Tanga kwa kushiriki kikamilifu katika mafunzo hayo, akibainisha kuwa ushiriki wao unaakisi weledi na utayari wa wataalamu wa afya kusimama mstari wa mbele katika kulinda afya za wananchi na kukabiliana kwa ufanisi na majanga pamoja na milipuko ya magonjwa.
Akizungumza kwa niaba ya washiriki wa mafunzo hayo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Dkt. Fani Mussa ameishukuru Wizara ya Afya,