Customer Feedback Centre

Ministry of Health

WIZARA YA AFYA YAWAITA WADAU WAKE KUELEKEA DIRA YA TAIFA 2050

Posted on: July 6th, 2024Na WAF, DAR ES SALAAM 


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, amesema baadhi ya wananchi waliohojiwa na tume inayotayarisha Dira ya Taifa 2050 wametaka suala la kuboresha huduma za afya liwe kipaumbele.


Mhe.Prof.Kitila ameyasema hayo leo Julai 06, 2024 wakati akifungua Kongamano la wadau wa Sekta ya Afya kuhusu maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 lililoandaliwa na Wizara ya Afya kwa wadau wake.


"Mhe. Waziri Ummy mimi nikushukuru sana kwakuwa Sekta ya kwanza kuandaa kongamano na kutualika kuja kuchukua maoni ya wadau wenu, ninyi kama sekta ndio mnawajua vilivyo wadau wenu" amesema Mhe. Prof. Kitila na kuongeza


"Kuwaleta wadau wenu kutatupatua uga wakukusanya kile ambacho ninyi kama wadau mnakiona kwa maslahi mapana ya Taifa tunapoelekea Diara ya Taifa 2050" amesisitiza Prof. Kitila


Mhe. Profe. Kitila amesema, wanachi waliohojiwa katika hatua za awali walisema Serikali imejidhatiti kuweka miundombinu ya afya na lililosalia sasa inatakiwa kuboresha huduma za Afya.


Awali Waziri wa Afya Mhe, Ummy Mwalimu akimkaribisha Mhe. Prof. Kitila Mkumbo alisema Sekta hiyo ni nyeti na kwa unyeti wake lazima kuzingatiwa katika Dira ya Taifa 2050


"Kwetu Sekta ya Afya, mbali yakuhudumia Vituo vilivyo chini ya Serikali lakini pia sekta binafsi inatuhusu, hivyo kosa dogo lazima litaliza alamu kwa Serikali ndio maana tukaona tuwe na Kongamano hili kwa wadau wetu" amesema Mhe. Ummy 


Waziri Ummy amesema Sekta ya Afya nchini imeendelea kutekeleza Dira ya Taifa ya 2025 inayomaliza muda wake, ambapo hadi kufikia sasa wamefanikiwa katika masuala kadha ikiwepo chanjo kwa kiwango kikubwa.


"Tumewafikia watoto 94 kati ya watoto 100 katika suala zima la Chanjo hii inatupatia morari na tutahakikisha malengo yanatimia ifikapo 2025 kwakuwafikia watoto 100" amesema Waziri Ummy


Awali akitoa Salaam za Ofisi ya Rais TAMISEMI, Naibu Waziri anaye shughulikia Afya Mhe. Dkt. Festo Dugange, ameiomba kamati hiyo kuzingalia suala lakuboresha huduma za Afya katika ngazi ya msingi.


"Dira ya Taifa 2050 ilenge Kuimarisha Huduma za Kibingwa na Ubingwa Bobezi hadi ngazi ya Wilaya ili kupunguza mzigo kwenye Hospitali za Mikoa na Kanda" amesema Mhe. DKT. Dugange 


Kongamano la kitaifa la wadau wa Sekta ya Afya limeandaliwa na Wizara ya Afya na kuwaalika wadau wake kwa ajili yakutoa Maoni itakayowezesha kuingizwa kwenye Dira ya 2050 kwa mustakabali wa Afya za watanzania. 


MWISHO