WIZARA YA AFYA YAIMARISHA UTAYARI WATAALAM WA MAABARA KUKABILIANA NA MAGONJWA YA MLIPUKO
Posted on: September 8th, 2026Na Zakayo Mosha-WAF Morogoro
Wizara ya Afya kupitia Idara ya huduma za Uchunguzi wa Magonjwa,kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO), linaendesha mafunzo kwa Wataalam wa Maabara wa Vituo vya Umma na Binafsi kutoka Mikoa ya Pwani, Tanga, Kilimanjaro, Mtwara, Lindi na Morogoro kwa lengo la kuimarisha utayari, usimamizi sampuli pamoja na utoaji wa taarifa sahihi za maabara ili kukabiliana na magonjwa ya mlipuko nchini.
Akifungua mafunzo ya Wataalam wa Maabara leo Septemba 8, 2026, mkoani Morogoro, Msajili Bodi ya Maabara Binafsi za Afya Bw.Dominic Fwiling'afu ametoa pongezi kwa Wizara ya Afya pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa kutambua na kuthamini mchango wa Sekta Binafsi katika utoaji wa huduma Bora za Afya kwa Wananchi.
"Napenda kuipongeza Serikali yetu kupitia Wizara ya Afya pamoja na WHO kwa kuona umuhimu wa ushirikiano wa Vituo vya Umma na Binafsi, hii ikiwa ni ishara muhimu kwamba Ufuatiliaji wa Magonjwa ni jukumu la mfumo mzima wa Afya na siyo la upande mmoja" amesisitiza Bw. Dominic
Amesema kuwa, vituo vya Umma na Binafsi vinapaswa kuendelea kufanya kazi kama mfumo mmoja ulio na lengo moja la kulinda Afya na uhai wa Mtanzania kupitia utoaji wa huduma bora za Afya.
Hata hivyo ameeleza kuwa, bodi hiyo itaendelea kusimamia utoaji wa huduma za afya unaozingatia sheria, Miongozo, viwa ngo vya ubora na usalama wa Mgonjwa.
"Ushiriki wa Sekta Binafsi katika Laboratory- Based Surveillance si jambo la hiari bali ni sehemu muhimu ya uwajibikaji wa kitaaluma na wa Afya ya Umma" amesema Bw.Dominic
Akihitimisha hotuba ya ufunguzi ametoa wito kwa Wataalam hao kutumia mafunzo watakayopata kuimarisha usimamizi wa sampuli,kuhakikisha wanatoa taarifa sahihi na kwa wakati pamoja na kufikisha kwa Watumishi wengine ujuzi na maarifa waliyopata ili kuendelea kulinda Afya za Watanzania.
Kwa upande wake Bw. Joakim John Chacha Mratibu wa huduma za Maabara sehemu ya Uchunguzi,Ufuatiliaji, na uthibiti wa Magonjwa kutoka Wizara ya Afya amesema kuwa, mafunzo hayo ni mwendelezo wa jitihada za Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) kuendele