Ministry of Health

SONGWE, MOMBA DC WAIMARISHA UTAYARI WA KUKABILIANA EBOLA NA ATHARI ZA EL NINO

Posted on: October 3rd, 2026

Halmashauri za Wilaya za Songwe na Momba, Mkoani Songwe leo Oktoba 2,2026, zimendelea na zoezi la kutathmini uwezo wao wa kukabiliana na ugonjwa wa Ebola na athari zinazoweza kusababishwa na El Nino, kupitia zoezi linalolenga kubaini mapungufu na maeneo yanayohitaji maboresho katika mifumo ya maandalizi na mwitikio wa majanga hayo.

Akizungumza kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Dkt. Calvin Mwasha, Mratibu wa Afya ya Mama na Mtoto, Lydia Kyumana, alieleza kuwa Halmashauri hiyo imejiandaa kukabiliana na majanga hayo mawili, huku akieleza kuwa tathmini hiyo ni muhimu katika kuonyesha maeneo yanayohitaji kuimarishwa.

“Sisi Wilaya ya Songwe tumejipanga vizuri kukabiliana na majanga haya mawili. Tunashukuru Serikali kwa kuona umuhimu wa kufanya tathmini hii, kwa sababu itatusaidia kujua mapungufu na madhaifu yaliyopo na maeneo tunayohitaji kuboresha zaidi ili kuepuka changamoto na athari zinazoweza kujitokeza,” alisema Kyumana.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba, Fabian Manoza, alieleza kuwa eneo hilo ni miongoni mwa maeneo yanayohitaji maandalizi ya mapema kutokana na changamoto zinazoweza kujitokeza wakati wa mvua.
“Eneo hili ni eneo hatarishi sana na tunashukuru kwa ujio wenu. Kwa upande wa Wilaya yetu, licha ya kuwa katika eneo hatarishi, tayari tumechukua hatua mbalimbali, ikiwemo kuunda kamati maalumu itakayosaidia katika kipindi hiki cha mvua inayotarajiwa,”alisema Manoza.

Aidha, Manoza alieleza kuwa Halmashauri imeendelea kutoa elimu kwa wananchi na kuwahimiza wanaoishi katika maeneo hatarishi kuhamia maeneo salama, huku akibainisha kuwa bado kuna umuhimu wa kupata nguvu zaidi kutoka kwa Serikali na wadau ili kuimarisha maeneo yenye changamoto za kijiografia.

“Bado kama Wilaya tunahitaji nguvu zaidi kutoka kwa Serikali na wadau. Hii itatusaidia kufanya maboresho katika maeneo yetu ambayo kijiografia yana hatari kubwa. Kwa upande wa Ebola, tulishajipanga,”alisisitiza Banoza.

Vilevile Mratibu wa zoezi hilo kutoka Wizara ya Afya Dkt.Francis Marwa amesema zoezi hilo linatekelezwa na Wizara ya Afya kupitia Sehemu ya Elimu ya Afya