WIZARA YA AFYA YAHUISHA MWONGOZO WA MATIBABU YA EBOLA NA MARBURG KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA
Posted on: September 29th, 2026Na Happyness Hans, WAF - Morogoro
Wataalamu wa afya nchini wamekutana kukamilisha kuhuisha mwongozo maalumu utakaotumika katika matibabu ya wagonjwa wa Ebola na Marburg, pamoja na namna ya kuzuia na kudhibiti maambukizi wakati wa kutoa huduma za afya, hatua hiyo inalenga kuongeza utayari wa nchi kukabiliana na magonjwa ya milipuko na kuhakikisha wagonjwa wanapata huduma stahiki, huku watoa huduma wakibaki salama.
Akizungumza leo Septemba 29, 2026, mkoani Morogoro, Dkt. Rodenta Bahegwa, Afisa wa Uimarishaji ubora, kukinga na kudhibiti maambukizi kutoka Wizara ya Afya, amesema kikao hicho kimeandaliwa na Wizara ya Afya kupitia Kitengo cha Dharura na Maafa pamoja na Kitengo cha Uhakiki wa kukinga na kudhibiti Maambukizi, kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO).
Amesema kikao hicho kimewakutanisha wataalamu kutoka Wizara ya Afya, TAMISEMI, Hospitali za rufaa za kitaifa, hospitali za kanda pamoja na hospitali zinazotoa huduma katika ngazi ya msingi,ameeleza kuwa lengo ni kuhakikisha mwongozo huo unazingatia mahitaji ya watoa huduma katika maeneo mbalimbali nchini.
Dkt. Bahegwa amesema mwongozo huo pia utawapa watoa huduma maelekezo sahihi ya namna ya kumhudumia mgonjwa endapo atapatikana na dalili za Magonjwa kama Ebola, Marburg au magonjwa mengine ya milipuko,
Aidha,amesema kuwa mwongozo huo umeandaliwa kwa kuzingatia Mwongozo Mama wa Kitaifa wa Matibabu pamoja na mapendekezo ya Shirika la Afya Duniani, ili kuhakikisha mgonjwa anayepata dalili anapatiwa matibabu sahihi na kwa wakati.
Amesisitiza kuwa, pamoja na matibabu, mwongozo huo umeelekeza pia hatua za kukinga na kudhibiti maambukizi (Infection Prevention and Control - IPC) ambapo watoa huduma wanapaswa kuzifuata wakati wa kumhudumia mgonjwa, amesema hatua hizo zinalenga kuhakikisha watoa huduma wanakuwa salama na kuzuia maambukizi kuenea wakati wa kutoa huduma kwa wagonjwa wa Ebola na Marburg.
“Mwongozo huu umejikita katika maeneo mawili muhimu, ambayo ni matibabu na afua za kukinga na kudhibiti maambukizi kwa watoa huduma, lengo ni kuhakikisha endapo magonjwa ya milipuko yatatokea nchini" amesema