Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

WADAU WAZIDI KUBISHA HODI KUCHANGAMKIA FURSA ZA UWEKEZAJI

Posted on: January 13th, 2026

Na WAF, Dodoma.


Wadau wa Sekta ya Afya kwenye uzalishaji wa bidhaa za afya (dawa na vifaatiba) wazidi kujitokeza kuonyesha nia ya ushirikiano na na Serikali katika upatikanaji wa uhakika wa bidhaa za afya na uwekezaji wa Viwanda vya dawa na vifaa tiba nchini.


Hayo yamedhihirishwa kupitia kikao cha Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa na Bw. Bw. Felix Ohnmacht, Mtendaji kutoka Kampuni ya Axess to Medicine yaliyofanyika katika ofisi za Wizara ya Afya jijini Dodoma, Januari 13, 2025.


“Lengo la kikao hiki lilikuwa kujadili namna ya upatikanaji wa rasilimali fedha zitakazochochea uwekezaji wa Viwanda vya dawa na vifaa tiba nchini, tumeelekeza mhusika kuunganishwa na kamati ya kitaifa ya kuharakisha na kurahisisha uwekezaji wa viwanda vya dawa pamoja na Bohari ya Dawa, ili kuboresha na kuharakisha mchakato wa huu” amesema Waziri Mchengerwa.


Kwa upande wake Bw. Felix amesema kuwa Kampuni ya Axess to Medicine (AXMED) imetenga kiasi Bilioni 25 kwaajili ya kuimarisha upatikanaji wa dawa hasa katika eneo la mama na mtoto kwa nchi saba za bara la afrika huku Tanzania ikitarajiwa kupata kiasi cha Shilingi Bilioni  5 kwa ajili ya manunuzi ya bidhaa za afya zitakazochagia katika kuboresha ubora wa huduma za matibabu na kinga kwa wananchi.


Katika hatua nyingine Waziri Mchengerwa amafanya mazungumzo na Bi. Doris Mollel, Mkurugenzi wa “Doris Mollel Foundation” aliyeambatana na Bw. Felix Ohnmacht, kujadili kuhusu uzinduzi wodi ya watoto wachanga inayotarajiwa kuzinduliwa Machi 2, 2026 katika Wilaya ya Kwimba, Mwanza.


Bi. Doris Mollel amesema kuwa ujenzi wa wodi hiyo ya watoto wachanga ni hatua muhimu katika kuboresha huduma za afya ya uzazi na mtoto, hususan kwa watoto wanaozaliwa njiti ambapo mradi huo utapunguza kwa kiasi kikubwa rufaa zisizo za lazima kwenda hospitali za Sekou-Toure au Bugando, na hivyo kuokoa muda na kuongeza nafasi ya watoto kupata huduma kwa wakati.