Wizara Ya Afya

TANZANIA YASISITIZA USHIRIKIANO WA EAC KUKABILIANA NA MAGONJWA YA MILIPUKO

Posted on: October 6th, 2026

Na Hassan Kimweri, WAF – Arusha

Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Florence Samizi, amesema nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zinapaswa kuendelea kuimarisha ushirikiano, mshikamano na kubadilishana taarifa kwa wakati ili kukabiliana na magonjwa ya milipuko na kuimarisha usalama wa afya katika ukanda huo.

Dkt. Samizi amesema hayo leo Oktoba 6, 2026 jijini Arusha wakati akizungumza katika Mkutano wa 26 wa Baraza la Mawaziri la Sekta ya Afya la EAC kwa niaba ya Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa ambapo Tanzania imeeleza umuhimu wa kuendelea kujenga uwezo wa pamoja katika kukabiliana na changamoto za afya zinazovuka mipaka.

"Tunapaswa kuendelea kujifunza kutokana na uzoefu wa Uganda katika kukabiliana na ugonjwa wa Ebola ikiwemo hatua za utambuzi wa mapema, usimamizi madhubuti wa wagonjwa, ufuatiliaji wa watu waliokutana na wagonjwa pamoja na uratibu wa kitaifa na kikanda ni muhimu katika kudhibiti milipuko," amesema Dkt. Samizi

Aidha, Dkt. Samizi amesema Tanzania inaendelea kufuatilia kwa karibu hali ya ugonjwa wa Ebola kufuatia mlipuko uliothibitishwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na nchi nyingine jirani ambapo kwa sasa hali ya Tanzania ni salama.

Katika hatua nyingine, Dkt. Samizi amesema Tanzania kwa kuonesha mshikamano na DRC, imetoa vifaa na bidhaa za tiba zenye thamani ya Shilingi milioni 220 kwa ajili ya kusaidia mwitikio wa mlipuko wa Ebola huku ikiendelea kuwa tayari kutoa wataalamu na msaada wa kiufundi katika maeneo mbalimbali ikiwemo ya ufuatiliaji, matibabu na huduma za maabara.

Hata hivyo, Dkt. Samizi amesema mkutano huo ni fursa muhimu ya kupitia utekelezaji wa maamuzi na maelekezo yaliyotolewa katika mikutano iliyopita ya Baraza hilo, kubaini changamoto na mapungufu yaliyopo na kukubaliana hatua za kipaumbele zitakazoharakisha utekelezaji wa mipango ya afya na kutoa matokeo yanayoonekana kwa wananchi wa EAC.

Mwisho, Dkt. Samizi ametoa wito kwa nchi wanachama kuendelea kudumisha mshikamano, ushirikiano na uwajibikaji katika kutekeleza maamuzi ya kikanda huku akisisitiza kuwa maamuzi yatakayofikiwa yanapaswa kuwa ya vitendo, yanayo