Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

HUDUMA ZA AFYA NCHINI ZIMEZIDI KUIMARIKA

Posted on: June 2nd, 2025

Na WAF, DODOMA

Serikali imesema katika kipindi cha Julai 2024 hadi Machi 2025, jumla ya wananchi 39,386,226 ya walihudhuria na kupata huduma katika vituo vya kutolea huduma za afya hapa nchini ikilinganishwa na wateja 38,031,200 waliopata huduma kipindi kama hicho kwa mwaka 2024.

Hayo yameelezwa Juni 2, 2025 na Waziri wa Afya, Mhe.
Jenista Mhagama wakati akiwaslisha Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/26.

Amesema kati ya hao, asilimia 8.2 walipata huduma kwenye ngazi ya Hospitali ya Taifa, Hospitali Maalum na Hospitali za Rufaa za Kanda, asilimia 11 ngazi ya hospitali za rufaa za mikoa, asilimia 15.9 hospitali za wilaya, asilimia 20.8 vituo vya afya na asilimia 37.5 katika ngazi ya zahanati, asilimia 4 ngazi ya kliniki,

Amesema asilimia 0.10 Maternity and Nursing Home na asilimia 2.4 ni vituo vinginevyo.
Amesema Takwimu za utoaji wa huduma za afya zinaonesha kwamba wananchi 56 asilimia 81 wanapata huduma katika ngazi ya afya ya msingi, hali hiyo inaonesha juhudi kubwa zilizofanywa na Serikali katika uwekezaji na uimarishaji wa huduma katika ngazi ya afya ya msingi na kuleta huduma karibu na wananchi