Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

GHALA LA MSD DODOMA KUSAMBAZA DAWA MIKOA JIRANI

Posted on: July 1st, 2025

Na WAF - Dodoma 


Ghala la kuhifadhia bidhaa za afya ikiwemo dawa lililojengwa mkoani Dodoma litasaidia kusambaza bidhaa hizo katika mikoa jirani ikiwemo Singida ili kurahisha upatikani wa bidhaa hizo kwa wananchi. 


Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace Magembe amesema hayo leo Julai 1, 2025 wakati wa ziara fupi ya Mkuu wa Idara ya Usimamizi wa Ruzuku Bw. Mark Edington kutoka katika mfuko wa Dunia wa kupambana na UKIMWI, TB pamoja na Malaria (Global Fund) iliyofanyika katika bohari ya dawa (MSD) Dodoma. 


"Ujenzi wa ghala hili unaendelea lakini ni ghala ambalo litakua kubwa na litaweza kusambaza bidhaa za afya sio tu Dodoma lakini pia katika mikoa jirani ikiwemo mkoa wa Singida na hii ndio njia mojawapo ambayo tumeamua tujitosheleze kwenye upatikanaji wa dawa, vifaa na vifaa tiba," amesema Dkt. Magembe.


Aidha, Dkt. Magembe amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya imekuwa na ushirikiano wa muda mrefu na mfuko wa Dunia (Global Fund) wa kupambana na UKIMWI, Kifua Kikuu (TB) pamoja na Malaria, ikiwa ni pamoja na  upatikanaji wa dawa, vifaa na vifaa tiba," amesema Dkt. Magembe.


Amesema, katika eneo jingine wanaloendelea kushirikiana nao ni katika ujenzi wa maghala ya kuhifadhia bidhaa za afya ikiwemo dawa kupitia bohari kuu ya dawa (MSD) ambapo ujenzi wa ghala hilo unaendelea mkoani Dodoma.