WAZIRI UMMY ATETA NA BALOZI IRELAND KUHUSU UBORESHAJI SEKTA TA AFYA KUPITIA MFUKO WA AFYA WA PAMOJA
Posted on: June 4th, 2023
Na. WAF - Dar es Salaam
Waziri Ummy na Balozi wa Ireland nchini Tanzania Mhe. Mary O’Neillleo wamekutana leo June 4, 2023 na kufanya mazungumzo katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam
Katika kikao hicho Waziri Ummy na Balozi na Mhe. Mary O’Neill wamejadili masuala mbalimbali ya Ushirikiano katika kuendeleza Sekta ya Afya nchini hususani katika mfuko wa Afya wa pamoja (Health Basket Fund) na changamoto zinazoikabili Sekta ya Afya.
Aidha, Waziri Ummy ameweza kubainisha changamoto mbalimbali zinazoikabili Sekta ya Afya nchini na namna gani wameendelea kushirikiana na Ubalozi wa Ireland katika kuhakikisha changamoto hizo zinatatuliwa ikiwemo kuja na programu zinazoweza kuboresha Sekta hiyo katika utoaji wa huduma za afya.
Kwa upande wake Balozi wa Ireland Nchini Mhe. Mary O’Neill amesema nchi hiyo itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili Sekta afya ambapo wameanza utekelezaji katika mpango kazi wao wa mwaka 2022/2026.