WATUMISHI WATAKIWA KUTUNZA VIFAA VYA HUDUMA
Posted on: September 19th, 2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan amewataka watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi kutunza vifaa vya kutolea huduma za afya kwa wananchi kwani vimeigharimu Serikali fedha nyingi.
Rais Samia amesema hayo leo tarehe 19 Septemba 2023 wakati akiweka jiwe la msingi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi.
Hospitali hiyo imegharimu shilingi Bilioni 4.8 katika ujenzi wake pamoja na ununuzi wa Vifaa na tayari mpaka sasa imeshatoa huduma ya CT Scan kwa wananchi 108.
Aidha, uwekaji wa jiwe la msingi katika Hospitali hiyo umeenda sambamba na utoaji wa huduma za wagonjwa wa nje (OPD), Huduma za wagonjwa wa dharura (EMD), huduma za Radiolojia pamoja na huduma za CT Scan hivyo kuwaondolea kero wananchi wa mkoa huo kusafiri mwendo mrefu kufuata huduma hizo.