Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

RAIS SAMIA AFANYA MIUJIZA SEKTA YA AFYA

Posted on: September 15th, 2023

Na. WAF, Mtwara


Rais wa Jamhuri ya Muunganoi wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya miujiza katika sekta ya afya kwa kutoa zaidi ya shilingi Bilioni 24 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini Mtwara.


Kauli hiyo imebainishwa leo Mkoani Mtwara na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel wakati akitoa salamu katika Mkutano wa Hadhara wa Rais Samia na Wananchi wa mkoa wa Mtwara.


Dkt,. Mollel asema kuwa Rais samia amezindua Huduma katika hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini Mtwara ikiwepo mashine ya CT Scan na X Ray tatu ambazo zote hizo zina Ghalimu Bilioni 7.5 ya vifaa vyote vilivyopelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini Mtwara


Aidha amesema kuwa Rais samia amehakikisha fedha zote za dawa zinatoka kwa asilimia 100 na sasa umetoa Bilioni 17 kwa ajili ya ujenzi wa Bohari ya Dawa kanda ya kusini na ujenzi umeaanza 


Ameeleza kuwa Raisd Samia kwa mwaka wa fedha 2023/24 kwa mkoa wa Mtwara kwenye sekta ya afya ameleta Bilioni 22 na katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Mtwara kuna ujenzi unaendelea unaoghalimu Bilioni 9.3 na ujenzi umefikia asilimia 88 na kwa mantiki hiyo wanamtwara wamepata hospitali ya kisasa itakayowapa Huduma zote katika mkoa huo


“Mhe. Rais mpaka sasa Mkoa wa Mtwara una CT Scani mbili moja katika hospitali ya Rufaa ya Kanda na nyingine katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara ili moja ikipata changamoto nyingine inaendelea kutoa Huduma kwa wananchi wa ukanda wa kusini”, ameelaza Dkt. Mollel


Ameongeza kuwa kwa miaka miwili ya Rais Samia katika sekta ya afya ametoa Tilioni 6.7 ambayo imefanya mapinduzi makubwa katika sekta ya afya nchini kwa kununua CT Scan 32, X Ray za kisasa 199 na kufanya nchi kuwa na jumla ya X Ray 543.


“Hivyo kwa mtu aliyeko Tandahimba , Newala akipata Huduma ya X Ray tunauwezo wa kuunganisha na kusoma majibu yake kwa kutumia X Ray za kisasa zilizo simikwa katika hospitali zetu chini ya uongozi imara wa Rais Samia”, Ameelzea Dkt. Mollel


Vile vile amempongeza Rais Samia kwa kukabidhi magari matatu na moja wapo ya gari  hilo linaubora wa kutoa  huduma kwa mgonjwa  maututi (ICU).