MADAKTARI BINGWA WA RAIS SAMIA WAANZISHA NCU HOSPITALI YA WILAYA NKASI.
Posted on: October 4th, 2024
Na. WAF, Nkasi - Rukwa.
Madaktari Bingwa wa Rais Samia wamefanikiwa kuanzisha kitengo maalumu cha uangalizi wa watoto wachanga (NCU) katika Hospitali ya Wilaya ya Nkasi ambacho hapo awali hakikuwepo katika Wilaya hiyo.
Akizungumza kwa niaba ya Madaktari hao Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Watoto Dkt. Amos Rubeja amesema sisi kama timu tumejitahidi kuongeza nguvu katika Hospitali hii kwa kuanzisha (NCU) ambayo inaweza kuhudumia watoto wachanga wenye changamoto mbalimbali za kiafya, walio zaliwa kabla ya muda, wenye uzito mdogo na kuweka watoto vifuani wenye uzito mdogo (Kangaroo mothercare) katika Wodi ya Watoto.
"Baada ya kufanikisha kuanzisha Kitengo hicho mpaka jana tumepata watoto wawili mmoja alikua na kilo 1 ambae alizaliwa wiki ya 31 na mwingine alikua na kilo 1.3 aliyezaliwa wiki ya 32 na wote wanaendelea vizuri". Amesema Dkt. Rubeja
Pia Dkt. Rubeja amesema kutokana na ujio wao wamefanikiwa kugundua watoto wenye changamoto mbalimbali na kuweza kuwapa Rufaa katika Hospitali Za juu zaidi ili waweze kupatiwa matibabu.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Thomas Ndeule amesema ujio wa Madaktari hao umekuwa na manufaa makubwa kwa wananchi wote wa Nkasi kwa wananchi kupata huduma za Kibingwa na Bobezi wilayani hapo.
"Pasingekuwa na uwepo wa madaktari Bingwa wa Rais Samia tungelazimika kuwapa Rufaa wazazi wa watoto hawa kuwasafirisha kuwapeleka katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa lakini ujio wa madaktari hawa umetusaidia sana na mpaka sasa wanaendelea vizuri na wazazi wameshukuru sana kwa kupunguziwa gharama za matibabu." Amesema
Kwa niaba ya wananchi wa Nkasi mkoani Rukwa Bi. Anastazia Benedikto mkazi wa Namanyere amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kufanikisha uwepo wa Madaktari Bingwa hao katika Wilaya ya Nkasi na kuwasihi wananchi wa wilaya hiyo kujitokeza kwa wingi kwa siku zilizobaki kupatiwa Huduma hospitalini hapo