HUDUMA ZA RADIOLOJIA (CT SCAN) TANGA ZAPUNGUZA IDADI YA RUFAA
Posted on: August 25th, 2023
Na. Mwandishi Wetu, Tanga
Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Tanga Bombo, imefanikiwa kupunguza rufaa wa wagonjwa 100 hadi 15 kwa wiki mbili baada ya kuanza kutoa huduma za kibingwa za radiolojia (CT SCAN).
Hayo yamebainishwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Tanga Bombo, Dkt. Naima Zakaria wakati akielezea mafanikio ya hospitali hiyo katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan mkoani Tanga.
Amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuboresha sekta ya Afya kwa kuongeza huduma za kibingwa za radiolojia (CT SCAN) nchini ili kupunguza rufaa za kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Aidha Dkt. Naima amesema uwepo wa huduma za kibingwa za Radiolojia (CT SCAN) imesaidia kugundua magonjwa mbali mbali hivyo kupunguza rufaa ambazo zinawagharimu wananchi katika kusarifi na kufuata huduma katika hospitali za nchi jirani.
Vile vile Dkt. Naima ameongeza Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo inafanya huduma za kibingwa za Radiolojia (CT SCAN) kwa wagonjwa saba na kufanikisha kupunguza rufaa kwenda katika hospitali ya Taifa Muhimbili.