Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

DKT. MAGEMBE AZINDUA KARAKANA YA KUTENGENEZEA VIFAA TIBA

Posted on: October 24th, 2023


Na WAF, Iringa.


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt.Grace Magembe amezindua Karakana ya kutengenezea vifaa tiba ili viweze kudumu kwa muda mrefu na kuhudumia wananchi.


Dkt. Magembe amefanya uzinduzi huo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa baada ya kukamilika kwa jengo liliojengwa na shirika la Health Promotion and System Strengthening pamoja na kuweka vifaa vyote vinavyotakiwa katika karakana hiyo.


Aidha Dkt. Magembe amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan umefanya maboresho makubwa katika sekta ya Afya,ikiwemo ujenzi wa majengo na ununuzi wa vifaa na vifaa tiba ikiwemo Ct Scan na Digital X-ray 


Pia Dkt. Magembe ameelezea maboresho yaliyofanyika kuanzia ngazi ya Taifa mpaka zahanati ni Zaidi bilion 200 lengo likiwa ni kuendelea kuboresha utoaji wa huduma bora za afya kwa mwananchi.


Hata hivyo, Meneja wa mradi huo Ndg. Ally Kabby amesema kuwa karakana hiyo itasaidia vifaa tiba hivyo kuwa katika ubora na kuwasaidia wananchi kupata huduma za afya karibu na kuwaepushia gharama za matibabu kwa kufata huduma katika hospitali za Kanda, Rufaa na Taifa.

Kwa upande wake Kaimu Mganga mfawidhi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa Iringa Dkt.Scholastica Malangalila amemshukuru Naibu Katibu Mkuu 


Dkt. Magembe kwa kukagua huduma mbalimbali zinazotolewa katika hospitali hiyo,sambamba na kuwashukuru wadau wa HPSS waliojenga karakana hiyo ili kuendelea kusaidia kuboresha huduma za Afya kwa wananchi.