WATU ZAIDI YA 300 WAPATIWA HUDUMA ZA KIBINGWA NA BINGWA BOBEZI MPANDA
Posted on: October 11th, 2024
Na. WAF - Mpanda
Wananchi zaidi ya 300 wamepata huduma za matibabu ya kibingwa na ubingwa bobezi kutoka kwa timu ya madaktari bingwa wa Samia katika kambi iliyowekwa Hospitali ya Manispaa ya Mpanda ndani ya siku nne.
Hayo yamebainishwa na Daktari wa kutoa dawa za usingizi na ganzi salama kutoka hospitali ya rufaa kanda ya Mbeya, Dkt. Letisia Komba ambaye pia ni sehemu ya timu hiyo ya Madakatari wa Rais Samia walioweka kambi ya siku saba katika Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi kwa lengo la kuwahudumia wananchi na kutoa huduma za uchunguzi na matibabu kwa wananchi wa Manispaa hiyo.
“Tupo hapa hospitali ya Manispaa ya Mpanda ikiwa leo ni siku yetu ya nne tumeona mwitikio mkubwa sana kwa wananchi kwa ajili ya kupatiwa huduma hizi za kibingwa na ubingwa bobezi”. Ameeleza Dkt. Komba.
Amesema kwa muda wote waliokaa hapo wamehudumia wagonjwa takribani 300 ambapo wametoa huduma za upasuaji kwa ajili ya uzazi na kwa ajili ya upasuaji wa ina nyingine takribani 11 na wananchi wamefurahia sana huduma hizo kusogezwa karibu na wao.
“Mbali na hayo tumekuwa tukiwajengea uwezo watumishi wanatoa huduma za afya katika hospitali hii katika upande wa upasuaji, kuona wagonjwa, kliniki na wa wodini”. Amesema Dkt. Komba.
Vile vile amesema kuwa watumishi wa hospitali hiyo pia wamejengewa uwezo katika masula mbalimbali ya matibabu ya kibingwa ili kuendelea kuwahudumia wananchi na kupunguza rufaa zisizo za lazima kwenda Mkoani na kanda.
“Wamepokea vizuri yale yote ambayo tuliojaribu kuwafundisha hadi sasa tumeona manufaa kwasababu kuna wagonjwa ambao walikuwa wanatakiwa kupata rufaa lakini wamepata huduma hapa”. Ameeleza Dkt. Komba.
Aidha, amesisitiza kuwa Madaktari wa Manispaa ya Mpanda kutumia ujuzi wote waliopata kwa wao uwezo ili waendele kutoa huduma bora kwa wagonjwa na kupunguza rufaa za kwenda katika hospitali ya rufaa za Mikoa na Kanda.
Naye mmoja wa wananchi ambaye akutaka kutwajwa jina lake amesema anamshukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Uongozi imara wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha kuwasogezea huduma za kibingwa karibu