Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

WAANDISHI WA HABARI WAASWA KUELEZEA UMMA MAENDELEO YA SEKTA YA AFYA

Posted on: May 6th, 2025

Na WAF - Dar es Salaam

Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama amewaasa waandishi wa habari kuelezea umma wa Watanzania juu ya maendeleo ya sekta ya afya katika maeneo mbalimbali nchini kwakuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya makubwa katika sekta hiyo.

Waziri Mhagama ametoa rai hiyo leo Mei 06, 2025 katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es Salaam wakati akikabidhi zawadi ya pikipiki mpya yenye thamani ya Shilingi Milioni 3.4 kwa mshindi Bw. Ismaily Abbas Kawambwa ambaye ameshinda tuzo ya uandishi bora wa makala ya sekta ya afya kwa mwaka 2025.

"Sisi tumekuwa ni miongoni mwa sekta chache ambazo ambazo zimetendewa haki kwenye sekta ya habari, kuna baadhi ya waandishi waliojitokeza kupambania tuzo ya uandishi wa kuhabarisha wananchi masuala ya afya na Bwana Ismaily ndiye aliyeshinda tuzo hiyo," amesema Waziri Mhagama.

Aidha, Waziri Mhagma amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kujali wananchi wake kwa kuboresha sekta ya afya ambapo tumeweza kupumguza vifo vitokanavyo na uzazi kutoka vifo 556 hadi vifo 104 kwa kila vizazi hai laki 100,000.

"Mnakumbuka Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan alipata tuzo kutoka Gates Foundation ya Marekani kwa kufanya mambo mengi mazuri kwenye sekta ya afya ikiwemo kusaidia kupunguza vifo vya akina mama vinavyotokana na uzazi, tumetoka vifo 556 hadi 104 kwa vizazi laki 100,000," amesema Waziri Mhagama.

Amesema, Malengo ya kidunia yanataka ifikapo mwaka 2030, vifo vya akina mama wakati wa kujifungua viwe vimepungua hadi kufika vifo 70 kwa vizazi hai laki 100,000.