Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

TUENDELEE KUBORESHA UBORA WA HUDUMA ZA AFYA

Posted on: February 22nd, 2024

 zaidi ubora wa huduma za afya zinazotolewa katika Taasisi hiyo ili uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali uwe na tija katika huduma bora zinatolewa MOI.

Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt. Faustine Ndugulile leo Februari 22, 2024 akiiongoza Kamati hiyo kufanya ziara ya kuona hali ya utoaji huduma za Afya, maboresho ya miundombinu ya kutolea huduma ikiwemo na miradi ya afya inayotekelezwa na Taasisi hiyo.

“Tunawapongeza MOI, hongereni sana mko katika mwelekezo sahihi, Kamati imeridhika na hali ya utoaji huduma tunawapongeza sana, endeleeni kuboresha zaidi ubora wa huduma mnazozitoa hapa”amesema Dkt. Ndugulile.

Wajumbe wa kamati hiyo walipata fursa ya kutembelea kitengo cha radiolojia kinachojihusha na vipimo vya CT -Scan, MRI na X-Ray, pia walitembelea kitengo cha huduma za wagonjwa maalum na wa kimataifa, jengo la kusubiria wagonjwa na wodini, ambapo walipata nafasi ya kuwapa pole wagonjwa na kusikiliza maoni yao.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesisitiza Uongozi wa Taasisi ya Mifupa MOI kuweka usimamizi mzuri wa utoaji huduma kwa kuwasimamia vyema watumishi ngazi za chini yao.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Prof. Abel Mkabi amesema uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambao umewezesha kuboresha hali ya utoaji wa huduma katika Taasisi ya MOI.
“Kutokana na uwekezaji uliofanywa na serikali ya awamu ya sita, tumeweza kuongeza idadi ya oparesheni kufikia 30 hadi 40 kwa siku huko nyuma tulikuwa tunafanya operesheni 20, tunamshukuru Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan” amesema Prof. Makubi na kuongeza
“Tumeweza kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi kwa asilima 97 kwa wagonjwa wa ubongo na asilimia 99 kwa wagonjwa wa mifupa” amesema Prof. Makubi.