Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

SERKALI IMEENDELEA KUBORESHA MFUMO WA RUFAA KWA MAMA MJAMZITO

Posted on: August 1st, 2024



Na WAF- Dar es Salaam. 

Serikali kupitia Wizara ya Afya imeendelea kuboresha mfumo mzima wa Rufaa utaosaidia kufuatilia mjamzito tangu anapotoka kituo kimoja mpaka anaendelea kupata huduma katika kituo kingine, hali itayosaidia kupunguza changamoto zitokanazo na uzazi.


Kauli hiyo imebainishwa na Mkurugenzi wa Idara ya huduma za uzazi mama na mtoto Dkt. Ahmad Makuwani leo Agosti, Mosi, 2024 jijini Dar Es Salaam katika kikao na Wadau mbalimbali wa Sekta ya Afya (Technical Working Group V) kujadili namna bora ya kuboresha afya ya mama na mtoto ili kufikia malengo ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.


Dkt. Makuwani ameeleza kuwa Serikali chini ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan inaendelea kuona namna bora ya kuboresha upatikanaji wa takwimu, ikiwemo matumizi ya mfumo wa biometric utaosaidia kuhifadhi takwimu za wajawazito kipindi chote mpaka atapojifungua ili kusaidia kufanya maamuzi sahihi.


Aidha Dkt. Makuwani amesema, licha ya kazi kubwa ya kupunguza vifo vya mama na mtoto kuendelea kufanyika nchini, bado nguvu kubwa inatakiwa kuongezwa hasa katika Mikoa ambayo bado haifanyi vizuri katika jitihada hizo.