Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

SERIKALI, WADAU WAKABIDHI VIFAA KWA WAHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII ZAIDI YA 1,500 TOKA MIKOA MINNE NCHINI.

Posted on: January 26th, 2025

Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace Magembe amekabidhi vifaa vifaa vyenye thamani ya TZS 522,032,431, kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii zaidi ya 1,500 kwa Mikoa ya Kagera, Tabora, Mbeya na Geita.

Vifaa hivyo vilivyonunuliwa na Taasisi ya Benjamin William Mkapa (BMF) kupitia ufadhili wa Global Fund chini ya Wizara ya Afya vimetolewa Januari 24, 2025 kwa wahudumu wa Afya waliopo kwenye mafunzo katika Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Biharamulo ambapo tukio hilo limefanyika katika Kituo cha Afya Rukaragata

Dkt. Magembe amesemaa ujio wa vifaa hivyo utachangia, kuongeza hamasa miongoni mwa wahudumu hao wa ngazi ya jamii.

“Sisi tukifanya kazi vizuri kupitia vitendea kazi hivi tunavyovipokea leo kutoka BMF, Tanzania, itakuwa salama, ni kwasababu mtakuwa mnalinda, hakuna tutakachowapa kinachoendana na kazi yenu ila chochote tutakachowapa kipokeeni kama moyo wa shukurani,” amsema Dkt. Magembe.

Akizungumza kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Benjamini Mkapa Fiundation, Bw. Erick Msunyaro amesema BMF inaunga mkono jitihada na juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan za utekelezaji mpango wa wahudumu wa Afya ngazi ya jamii.

Amesema kuwa kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo  Global Fund na Irish Aid  katika awamu ya kwanza  jumla ya wahudumu wa afya ngazi ya jamii 1943 wanapatiwa mafunzo, ikiwa ni sehemu ya mpango wa kusomesha wahudumu wa afya ngazi ya jamii 4,747 kwa awamu tofauti.

“Sisi Benjamin William Mkapa Foundation tutaendelea kushirikiana na Serikali na wadau wa maendeleo katika kuhakikisha huduma za afya kwa jamii zinaboreshwa, hususani kwa makundi yaliyo pembezoni na yenye uhitaji mkubwa zaidi, lengo letu ni kuhakikisha kila Mtanzania anakuwa salama,” amesema Bw. Mnyasuro.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Ntuli Kapologwe amesema vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na fulana mbili, mwamvuli, kizibao, buti, begi la mgongoni, kipima joto, koti na koti la mvua kwa kila
mmoja.