Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

SERIKALI KUENDELA KUSHIRIKIANA NA WHO KUBORESHA SEKTA YA AFYA.

Posted on: August 2nd, 2024



Na WAF – DAR ES SALAAM

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. John Jingu Amesema serikali kupitia Wizara ya Afya itaendelea kushirikiana na Wadau wa maendeleo katika sekta ya afya nchini akiwemo Shirika la Afya Duniani WHO ili kuhakikisha watu wote wanapata huduma bora za afya.

Dkt. Jingu ameyasema hayo Agosti 2, 2024 Jijini Dar es salam Wakati makabidhiano ya vitanda 65 vya wagonjwa wa kipindupindu kutoka WHO kwenda Tanzania ikiwa ni sehemu ya lengo la kuimarisha Mapambano dhidi ya Magonjwa ya Mlipuko Nchini kwa sasa na yajayo ikiwemo kipindupindu na dharura kama hizo nchini Tanzania.

Dkt. Jingu amesema mashirikiano baina ya Wizara ya Afya na WHO yanalenga kuimarisha mashirikiano katika kuwajengea uwezo watoa huduma za Afya na kuimarisha miundombinu ya kutolea huduma za afya nchini ili kufikia lengo la utoaji wa huduma bora za Afya Nchini..

“WHO mmekuwa wadau Muhimu Katika eneo hili na kuhakikisha watu wote wanapata huduma nzuri za Afya, Moja ya mambo ni kuhakikisha tunawajengea uwezo wataalam wetu kwa kuwapatia mafunzo stahiki, nakuhakikisha tuna miundombinu mizuri pamoja na viafaa vyote na mahitaji yatayosaidia huduma husika ziweze kutolewa, na leo hapa tunapokea baadhi ya vifaa hivyo ambavyo vitawezesha watoa huduma wetu kutimiza majukumu yao” amesema Dkt. Jingu.

Ameongeza kuwa mashirikiano hayo pia yanakuwa chachu ya utayari wa muda wote wa pamoja wa kupambana na magonjwa yanayolipuka nchini ambapo WHO wamekuwa wadau wakubwa na Serikali inajivunia Kushirikiana nao.

Aidha Dkt. Jingu amewashukuru WHO kwa kuwa na utayari wa muda wote na kuendelea kushirikiana na wizara ya afya na Serikali ya Tanzania Kwa Ujumla na kuwasihi kuendelea kufanya hivyo ili kuchochea matokeo chanya katika sekta ya afya nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa WHO Nchini (Tanzania) Dkt. Charles Sagoye – Moses amesisitiza kuwa wito wao ni kuimarisha na kuendelea na utekelezaji wa mbinu mbalimbali za kisekta za kuzuia na kudhibiti magonjwa ya mlipuko nchini ikiwemo Kukomesha kipindupindu kwa kushirikiana na Serikali na jamii nzima.