MADAKTARI BINGWA WAFANIKIWA KUTOA BANDAMA YENYE SENTIMITA 18 KUNUSURU MAISHA YA MTOTO
Posted on: October 24th, 2025Na WAF - Nyamagana, Mwanza
Madaktari Bingwa wa Rais Samia wamefanikiwa kumfanyia upasuaji mtoto mwenye umri wa miaka 11 aliyekuwa akisumbuliwa na tatizo la bandama kubwa yenye urefu wa zaidi ya sentimita 18 katika Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana, jijini Mwanza.
Upasuaji huo umefanyika Oktoba 22, 2025, chini ya Daktari Bingwa wa Upasuaji, Dkt. Jonathan Boniventura, wakati wa kambi ya Madaktari Bingwa wa Rais Samia inayoendelea jijini humo.
Mama wa mtoto huyo, Bi. Latifa Hamza, amesema mtoto wake alianza kuugua akiwa na umri wa miaka mitatu, na tatizo hilo lilianza taratibu hadi alipobainika kuwa na upungufu wa damu na tatizo la selimundu.
“Kila baada ya miezi miwili tulilazimika kumpa damu chupa mbili kwa sababu damu ilikuwa inapungua mara kwa mara. Bandama yake nayo ilikuwa inaendelea kukua,” amesema Bi. Latifa huku akishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kambi hizo za madaktari bingwa ambazo zimeokoa maisha na gharama kwa wananchi.
Kwa upande wake, Dkt. Boniventura amesema mtoto huyo alifika hospitalini akiwa na upungufu mkubwa wa damu, huku bandama yake ikishindwa kufanya kazi ipasavyo kutokana na chembe nyekundu za damu kugandana kwa sababu ya umbo la selimundu.
“Mtoto huyu alikuwa ameongezewa damu zaidi ya mara 24, na ukubwa wa bandama ulimletea maumivu makali ya tumbo. Upasuaji umefanikiwa, na mtoto anaendelea vizuri,” amesema Dkt. Boniventura.
“Umri wa miaka 11 haitakiwi kuzidi 10cm wakati mgonjwa wetu ilikuwa na zaidi ya 18cm. Bandama inafanya kazi katika mfumo wa tezi katika mwili( lymphatic system). Inatengeneza kinga ya mwili na kuhifadhi chembe nyekundu za damu. Kwa wagonjwa wenye seli mundu wanapata changamoto ya kuvimba bandama kwa sababu hizi seli mundu zinaziba mishipa ya damu inayaruhusu damu kutoka kwenye bandama mara kwa mara," amefafanua Dkt. Boniventura
Ameongeza kuwa hali hiyo husababisha bandama kuugua, kuvimba na maumivu makali sana. Matibabu yake ni kuiondoa na kumpa dawa za kinga ya kupambana na bakteria.
Kambi ya Madaktari Bingwa wa Rais Samia inaendelea kutoa huduma mbalimbali za kibingwa kwa wananchi wa Mkoa wa