Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

MADAKTARI BINGWA WA RAIS SAMIA WAENDELEA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA SONGWE

Posted on: September 30th, 2024

Na WAF - Songwe

Dhamira ya Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuboresha huduma za Afya katika Mkoa wa Songwe kupitia kwa madaktari bingwa wa Rais Samia ambapo lengo kuu likiwa ni kuingia na kutoka katika nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).

Katibu Tawala wa Mkoa Bi. Happiness Seneda amesema hayo leo Septemba 30, 2024 wakati wa kuwakaribisha wataalamu hao akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa Songwe amnapo amesema mkoa huo umepiga hatua kubwa katika Sekta ya Afya ikiwa ni pamoja na kuwekeza katika hospitali ya mkoa na wilaya.

“Mkoa huu hadi kufikia mwaka 2015 ulikuwa na hospitali Mbili tu za Halmashauri lakini sasa Halmashauri zote Tano zimejengewa hospitali na zimeanza kutoa huduma mbalimbali ikiwemo za mama na mtoto." Amesema Bi. Seneda

Amesema, kwa upande wa vituo vya afya, kabla ya mwaka 2015 mkoa ulikuwa na kituo cha afya Kimoja kilichokuwa kinatoa huduma za upasuaji wa dharura lakini sasa kuna jumla ya vituo vya afya Nane vyenye uwezo wa kutoa huduma za upasuaji hivyo kufanya jumla ya vituo vyenye uwezo wa kutoa huduma hizo kufikia 18.

Aidha, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa fedha zilizowezesha Mkoa huo kutoa huduma za mionzi kwenye vituo 13 ikiwemo huduma za CT-Scan zilizoanza kutolea kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo wa Songwe.

"Tunamshukuru Rais Samia kwa maono yake katika kuboresha Sekta ya Afya, wananchi tuendelea kuiunga mkono Serikali katika juhudi zake za kutafuta afya bora kwa wote lakini pia nawapongeza watumishi wa Sekta hii kwa kazi yenu ngumu ya kuwahudumia wananchi." Amesema Bi. Seneda

Kwa upande wake Mratuibu wa kambi hiyo kutoka Wizara ya Afya Ndg. Fidea Obimbo amesema kambi hiyo inatoa fursa kwa wananchi, hususani wale wanaoishi katika maeneo ya Songwe na mikoa jirani kupata huduma za kibingwa bila ya kusafiri umbali mrefu.

Ndg. Obimbo amesisitiza kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameona umuhimu wa kuwafikia wananchi katika ngazi za chini ambazo zinaweza kutopata huduma hizo mara kwa mara.