Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

KITUO CHA UMAHIRI MATIBABU YA SARATANI KUJENGWA NCHINI TANZANIA

Posted on: February 6th, 2024



Serikali ya Tanzania leo Februari 6, 2024 imeingia Mkataba wa makubaliano na Taasisi ya Global Health Catalyst ya nchini Marekani kwa ajili ya ujenzi na uanzishwaji wa Kituo cha Umahiri wa Matibabu ya Saratani hapa nchini.

Katika Mkataba huo ambao kwa Tanzania umesainiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afua Dkt. John Jingu, na Mkurugenzi wa GHC Prof Wil Ngwaa, Tanzania inatarajiwa nchi pekee katika Ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara kuwa na kituo chenye uwezo wa kutoa huduma za kibingwa bobezi zaidi katika matibabu ya Saratani.

Tukio hilo limeshuhudiwa mbele ya Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu pamoja na Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hassan Hamis Hafidh pamoja na Watalaam na Wadau wa Sekta ya Afyaleo Februari 06, 2024 Jijini Dar Es Salaam.

Hizi ni jitihada endelevu za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suhulu Hassan za kuendelea kuhakikisha Huduma bora na za kibingwa zinapatikana hapa hapa nchini na kuendelea kukuzw utalii wa tiba na kuvutia mataifa jirani kufuata huduma za matibabu nchini.