Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

KITUO CHA KUTOLEA MAFUNZO KWA NJIA MTANDAO CHAZINDULIWA

Posted on: July 26th, 2022

Na. WAF - Dar es Salaam

Kituo cha mafunzo kwa njia ya mtandao kwa Watumishi wa Afya ambacho kitasaidia kukabiliana dhidi ya magonjwa mbalimbali ikiwemo ugonjwa wa UVIKO-19 kimezinduliwa ikiwa ni ishara ya kuanza kwa huduma katika kituo hicho.

Kituo hicho kimezinduliwa leo Julai 26, 2022 na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa kituo cha kudhibiti magonjwa cha Marekani (CDC) Dkt. Rochelle Walensky na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt. Donald Wright katika hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Akiongoza uzinduzi huo, Waziri Ummy amesema, kuna vituo nane na vituo vingine vidogo vidogo 272 ambavyo vinashirikiana katika kutoa maarifa kwa Watumishi wa Afya katika kuwahudumia wagonjwa.

Amesema, vituo hivyo vinasaidia kupata miongozo ya jinsi ya kutoa matibabu kwa wagonjwa na kupunguza Rufaa ambazo zinaweza kuepukika kwa kumhudumia mgonjwa katika kituo hicho bila kumpeleka katika hospitali ya Muhimbili.

Sambamba na hilo, Waziri Ummy, ameishukuru CDC kwa kuendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali, hususan katika kutoa mafunzo ya njia bora za kupambana dhidi ya maambukizi, jinsi ya kumhudumia mgonjwa na jinsi ya kufanya vipimo.

"Kwa niaba ya Serikali tunaishukuru CDC kwa kuendelea kutuunga mkono, kituo hiki kitatoa mafunzo ikiwemo jinsi ya kudhibiti maambukizi, jinsi ya kumuhudumia mgonjwa na jinsi ya kufanya vipimo na kugundua mgonjwa anaumwa nini ." Amesema Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy amesema matokea mazuri yanayopatikana kwa Watanzania kuchanja ni kutokana na ushirikiano kati ya Tanzania na CDC ambapo hadi kufikia Julai 25, 2022 chanjo ya UVIKO-19 imetolewa kwa watu Mil. 12.8 ambayo ni sawa na 41.8% kwa lengo la kufikia 70% ya Watanzania wenye umri wa miaka 18 na kuendelea.

Mbali na hayo Waziri Ummy amesema, kupitia ushirika huo na CDC umewezesha Serikali kupata maabara 44, kufundisha Wataalamu wa maabara takriban 556 katika maswala ya microbiology and udhibiti ubora (quality management).

Kwa upandemwingine, Waziri Ummy ameishukuru Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Kituo cha kudhibiti Magonjwa cha Marekani (CDC) na Mhe. Balozi Wright