AFYA WAMALIZA NANE NANE 2024 KWA KISHINDO, WAHUDUMIA WANANCHI ZAIDI YA 14,000
Posted on: August 12th, 2024
Na WAF Dodoma
Wizara ya Afya imekuwa moja ya Wizara iliyofanya vizuri kwenye Maonesho ya Nanenane 2024 kwa kuhudumia wananchi zaidi 14,000 waliojitokeza katika Mabanda ya wizara hiyo na taasisi zake na kutwaa tuzo ya mshindi wa tatu wa Wizara Mtambuka zilizofanya vizuri wakati wote wa Maonesho.
Kwa mujibu wa takwimu zinaonesha mara baada yakukamilika kwa Maonesho hayo wingi wa wananchi walijitokeza walifika kupata chanjo ya Homa ya Ini wakiwepo 527 walipata chanjo aidha waliogundulika na Homa ya ini wapatao 53 walipewa rufani kwa ajili matibabu kabla yakupatiwa chanjo hiyo.
“Wananchi elfu 13077 wajitokeza, na wengine kupatiwa mipira ya kiume (Condom) zipatazo 2937 ziligawiwa kwa wananchi.
Kwa upande wa shinikizo la damu waliopima walikuwa elfu 5000 huku, 1663 walifanikiwa kupima Kifua Kikuu na waliogundulika na maambukizi walikuwa wawili ambao wote wameanzishiwa matibabu ya dawa.
Kwa upande wa waliojitokeza kupata elimu ya uzazi wa mpango walikuwa wananchi 260 na baadhi ya njia za uzazi walizo shauriwa ni ni pamoja na sindano, vidonge, vipandikizi, condom na kitanzi/lupu.
Huduma zilizotolewa katika muda wa siku zote kumi ni pamoja na Uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi, Elimu ya afya na ugawaji vipeperushi, uchunguzi wa Kifua kikuu (TB), Elimu ya uzazi wa mpango , upimaji wa maambukizi ya virusi vya UKIMWI, Elimu na uchunguzi juu ya afya ya Akili, upimaji wa shinikizo la damu pamoja na upimaji na ugawaji wa chanjo ya Homa ya Ini na Uviko 19 na pamoja na elimu juu ya Tiba asili na tiba lishe
Afisa Habari Mwandamizi kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Afya Atley Kuni, amesema kuwa Banda la Wizara ya Afya katika maonesho hayo zilikuwepo pia Taasisi zilizochini ya Wizara ambazo ni taasisi ya Muhimbili Orthopedic Institute, Hospitali ya Benjamin Mkapa Mamlaka ya vifaa Tiba na dawa TMDA, NHIF, Baraza la Uuguzi na Ukunga TNMC, pamoja na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali