Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

WAZIRI WA AFYA UMMY MWALIMU ATEKELEZA AGIZO LA MAKAMU WA RAIS KUMTAKA KUFIKA UKEREWE KUFUATILIA MGOGORO WA UJENZI WA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA UKEREWE.

Posted on: December 20th, 2022

Waziri wa Afya Mhe. @UmmyMwalimu leo akiwa njiani kutokea Jijini Mwanza kuelekea katika Visiwa vya Ukerewe kufuatia agizo alilotoa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Phillip Isdor Mpango mnamo Novemba 25, 2022 la kumtaka Waziri Ummy Mwalimu kufika katika Kisiwa cha Ukerewe na timu yake kuchunguza mgogoro wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Ukerewe na kuchunguza ubadhirifu wa fedha za mradi huo. Katika safari hiyo Waziri Ummy Mwalimu ameongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Adam Malima.