Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

Watanzania wanyakua tuzo ya umahiri uandishi habari za afya ya uzazi - Afrika

Posted on: January 13th, 2022

Na Mwandishi Maalum

Wanahabari watatu wa Tanzania wameibuka kidedea katika tuzo za umahiri uandishi wa habari kuhusu afya ya uzazi, Barani Afrika za 'Merck More Than a Mother - 2021},

Waandishi hao ni Veronica Mrema wa Matukio na Maisha Blog ambaye ameshinda katika kipengele cha vyombo vya habari mtandaoni.

Wengine ni Christina Mwakangale wa Nipashe/Guardian kipengele cha magazeti na Adam Gabriel {Hhando, wa CG FM}, kipengele cha redio.

 Tuzo hiyo inaangazia masuala ya afya  uzazi Barani Afrika, Shirika la Merck Foundation la Ujerumani kwa kushirikiana na Marais na Wake wa Marais Barani Afrika, limetangaza.

Zinafanyika mwaka wa nne sasa mfululizo tangu zilipoanzisha 2017/18. Hii ni mara ya tatu kwa Veronica kuwania na kutwaa tuzo hiyo, zinalenga kuhamasisha wanahabari kuelimisha jamii kuachana na mila potofu na vitendo vya unyanyapaa kwa watu waliokosa watoto {wagumba/tasa}.

Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Seneta Dk. Rasha Kelej, ametangaza majina ya washindi wa tuzo hiyo kupitia taarifa yake iliyotumwa kwa vyombo vya habari.

Pamoja na Watanzania hao walioshinda katika Ukanda wa Afrika Mashariki, wametangaza pia washindi wengine kutoka Ukanda wa nchi za Kusini mwa Afrika, Afrika Magharibi na nchi ambazo zinazungumza lugha ya Kifaransa.

Seneta Kelej ambaye pia ni Rais wa shirika hilo linaloshirikiana na marais wa barani Afrika, amesisitiza "Nina furaha kuwatangaza washindi hawa wa Merck Foundation Africa Media Recognition Awards ‘More Than a Mother’ 2021 {zaidi ya Mama}.

“Pia nachukua fursa hii kuwashukuru m

Marais wa Afrika kwa nia yao thabiti na kushirikiana nasi kama Mabalozi wa Merck Foundation.

Amevipongeza pia vyombo vya habari Barani Afrika ambavyo vimekuwa sauti ya wasio na sauti na kuongeza uelewa kwenye jamii hususan unyanyapaa kwa wagumba, tasa katika changamoto za kupata watoto.

Ameongeza "Kila mara jukumu kuu la vyombo vya habari, vina uwezo wa kuleta mabadiliko ya kitamaduni katika jamii zetu kwa njia ya gharama nafuu.

"Ninawakaribisha washindi wote kuwa wanachama wa walimu wetu wa Merck Foundation na kufanya kazi kwa karibu nasi, ili kuunga mkono, kuwawezesha wanawake na wasichana katika ngazi zote.”

“Nimefurahishwa na kazi iliyoonyeshwa na washindi wetu wote, inanipa furaha kubwa kutangaza kwamba Merck Foundation inawazawadia washindi program ya mwaka mmoja 'MasterClass'

Amesema kozi hiyo itawajengea washindi hao uzoefu wa kipekee wa mtandaoni na kujifunza ya haraka ambayo hufikiwa popote kwa njia ya mtandao.

Ningependa kutoa wito wa kuwasilisha maombi Merck Foundation Africa Media Recognition Awards 'Zaidi ya Mama' kwa mwaka 2022," ametoa rai.

MWISHO