WATANZANIA 700 KUFANYIWA UCHUNGUZI WA MOYO BMH
Posted on: February 13th, 2024 
 
                                
                            
	
	
Watanzania 700 wanatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa moyo kwenye kambi ya moyo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) jijini Dodoma.
	
	
Daktari Bingwa Moyo wa BMH, Dkt Calvin Masava, amesema hayo leo ambapo amesema kuwa BMH inashirikiana na madaktari sita kutoka Netherlands kufanya kambi hiyo ya moyo.
	
	
"Lengo la kambi mbali na kutoa huduma lakini inalenga kubadilishana uzoefu na wenzetu kutoka Netherlands," ameeleza Dkt. Masava
	
	
Dkt . Masava amefafanua kuwa watakaokutwa na matatizo ya moyo watapatiwa matibabu hapa hapa BMH.
	
	
Hata hivyo amesema kuwa hiyo ni kambi yao ya kwanza ya pamoja na wenzao kutoka nje kwa mwaka huu.