Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

WADAU WATAKIWA KUWEKEZA NGUVU YA PAMOJA MAPAMBANO YAKUTOKOMEZA FISTULA

Posted on: May 21st, 2024

Na WAF, ARUSHA

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Afya ya Mama na Mtoto kutoka Wizara ya Afya Dkt. Mzee Nassor amewataka wadau wa Fistula, kuendelea kuunganisha nguvu za pamoja kwenye mapambano dhidi ya tatizo hilo ili kutokomeza kabisa.


Dkt. Mzee ameyasema hayo Mei 21, 2024 Jijini Arusha wakati wa kikao kazi cha kupanga mikakati ya pamoja ya kukabiliana na ugonjwa wa Fistula na Wizara ya za Kisekta na wadau wa maendeleo.


Dkt. Mzee amesema Serikali imeimarisha huduma za Afya kwa ngazi zote na kuthibitisha hilo ni pamoja na kupungua kwa vifo vya vya uzazi kwa asilimia 80.


"Nitumie kikao hiki kuendelea kuwahimiza wanawake kujitokeza mapema kwenye vituo vya afya ili kuanza Kliniki ya mapema hali itakayo wezesha kukabilina na tatizo la uzazi hatarishi unaweza kusababisha tatizo la Fistula " amesema Dkt. Mzee.


Dkt. Mzee amesema, wataendelea kufanya tafiti na kutambua maeneo yalio athirika kwa ukumbwa na wagonjwa wa Fstula kwa wingi ili kuongeza nguvu ya mapambano.


Akitoa Salaam za mkoa, Mganga Mkuu wa mkoa wa Arusha, Dkt. Charles Mkumbaveka, amesema, mkoa huo kwa sasa upo salama na hakuna magonjwa yoyote ya mlipuko.


"Ninawapongeza sana kuuchagua mkoa wa Arusha kuwa mwenyeji wa mkutano huu, Mhe. Paul Makonda anawasalimu lakini amewashukuru kwakuchagua mkoa wetu kuwa mwenyeji wa maadhimisho hayo kitaifa.


Akiwa katika kikao hicho cha maandalizi Dkt. Mzee amesema, Serikali inafanya jitihada mbalimbali ili kuhakikisha huduma za afya zinazidi kuimarika na moja ya nyenzo wanayotumia kwa sasa ni zoezi la Madaktari Bingwa linalokwenda sambamba na kuwajengea uwezo watendaji wa afya hadi ngazi ya Wilaya.


Maadhimisho ya Siku ya Fistula yanatarajiwa kufanyika mkoani Arusha Mei 23, 2024 na kuongozwa na kauli mbiu Vunja Minyororo, Zuiya Fistula Tanzania.