Wizara Ya Afya

VIPAUMBELE 11 KUIBEBA WIZARA AFYA BAJETI, 2026/27

Posted on: May 11th, 2026

Na Atley Kuni, WAF-Dodoma

Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema Serikali imejipanga kuendelea kuboresha Sekta ya Afya nchini kupitia utekelezaji wa vipaumbele mbalimbali vitakavyoongeza upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi mijini na vijijini.

Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha Mapitio ya Bajeti ya mwaka 2025/26 na Makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Afya kwa mwaka wa fedha 2026/27.

Mhe. Mchengerwa amesema Serikali imeelekeza nguvu katika kuboresha huduma za afya, ikiwepo bima ya afya kwa wote, kuongeza wataalam pamoja na kuimarisha matumizi ya teknolojia katika hospitali na vituo vya kutolea huduma za afya.

"Serikali itaendelea kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora zenye staha na utu kwa kuboresha mazingira ya utoaji huduma, kupunguza muda wa kusubiri matibabu na kuimarisha mifumo ya kushughulikia malalamiko ya wananchi katika vituo vya afya", amesema Mhe.Mchengerwa.

Katika kuwapunguzia wananchi mzigo wa gharama za matibabu, Waziri Mchengerwa amesema Serikali itaendelea na utekelezaji wa Mpango wa Bima ya Afya kwa Wote kwa kusajili kaya zenye uhitaji pamoja na kuhamasisha wananchi wengi zaidi kujiunga na huduma hiyo muhimu.

Aidha, Serikali imepanga kuongeza uwekezaji katika viwanda vya ndani vya dawa na bidhaa za afya ili kuhakikisha upatikanaji wa dawa muhimu unaimarika na kupunguza utegemezi wa bidhaa kutoka nje ya nchi.

Waziri Mchengerwa amefafanua kuwa Serikali inatarajiwa kuongeza ajira na kukuza uchumi wa ndani, sambamba na kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika Sekta ya Afya kwa kuunganisha mifumo ya taarifa za afya, kuongeza huduma za afya mtandao pamoja na matumizi ya akili unde kwenye kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Katika upande wa huduma za kinga, Mchengerwa amesema, Serikali imeweka mkazo kwenye mapambano dhidi ya magonjwa ya mlipuko, magonjwa yasiyoambukiza pamoja na kuendelea kuimarisha huduma za chanjo nchini.

"Katika Mwaka ujao wa fedha wahudumu wa afya ngazi ya jamii 8,000 wanatarajiwa kuajiriwa ili kuongeza huduma za afya kwa wananchi maeneo mbalimbali nchini.

Kwa upande wa afya ya uzazi, mama na mtoto, Serikali imeahidi kuon