Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

TANZANIA YAPOKEA SHEHENA YA CHANJO YA UVIKO-19 AINA YA SINOPHARM

Posted on: December 8th, 2021
Akiongea wakati wa mapokezi ya chanjo hizo,Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima amesema chanjo hizo zimekuja na hivyo kuwapatia wananchi gursa ya kuchagua chanjo anayotaka kwani chanjo hizo ni salama ,zina ufanisi na ubora uliokubalika kisayansi na zimeonesha mafanikio makubwa katika kupunguza makali ya ugonjwa na kueousha kifo.
 
“Ni dhahiri kuwa Serikali ya Tanzania imeonesha nia njema ya kuendelea kuwajali wananchi wake kana ambavyo imekuwa ikifanya siku zote kwenye sekta mbalimbali ikiwemo eneo la afya”.
 
Hata hivyo Dkt. Gwajima amesema Serikali inategenea kupokea chanjo za aina zingine katika wiki zijazo na itaendelea kuyoa taatifa na utaratibu wa kila inapopokea ili wananchi wafahamu.
 
Kwa upande wa watanzania waliochanjwa Waziri huyo amesema hadi kufikia tarehe 7 Oktoba takwimu zinaonyesha wanachi waliochanjwa wamefikia 760,962 sawa na asilimia 74.4 kwa Tanzania Bara na 10,800 Zanzibar na kuongeza kuwa mwitikio ni mkubwa na chanjo za awamu ya kwanza zinatarajia kumalizika mwisho wa wiki ijayo.
 
Aidha, Dkt.Gwajima ametumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kuendekea kusikiliza Serikali na Wataalamu wa afya na kujiepusha na habari zisizo rasmi”niwaombe tuwe makini na kusikiliza maelekezo tunayopewa na Wizara ya Afya hususani katika kujikinga na janga hili la kitaifa”.
 
Vilevile Dkt. Gwajima aliwasisitiza viongozi ba watendaji wa ngazi zote kuendelea kutoa ushirikiano ili kuhakikisha kuwa wqnanchi wanaendelea kuelimishwa na kuhimizwa kwenda kwenye vituo vya huduma za afya ili wakapate elimu kuhusu umuhimu wa chanjo.