Wizara Ya Afya

TANZANIA, GAVI KUENDELEA KUIMARISHA HUDUMA ZA CHANJO NCHINI.

Posted on: September 21st, 2026


Na Zakayo Mosha- WAF DODOMA

Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya itaendelea kushirikiana na Muungano wa Kimataifa wa utoaji wa huduma za chanjo kwa kushirikiana na Global Alliance for Vaccine and Immunization (GAVI) hapa nchini kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma za chanjo ili kulinda Afya za Wananchi.

Kauli hiyo imetolewa leo Septemba 21,2026 Jijini Dodoma katika Ofisi za Wizara ya Afya na Bw. Emmanuel Tayari Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Dawa na Vifaa Tiba ambaye amemuwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe, alipokutana na wadau wa shirika la GAVI hapa nchini ili kupitia utekelezaji wa miaka mitano (2021-2025) wa shughuli za chanjo nchini.

Bw.Tayari amesema ushrikiano huo ulianza zaidi ya muongo mmoja uliopita na hadi sasa zaidi ya dola za marekani milioni 597 zimetumika kuboresha huduma za chanjo, amesema Tanzania imepata mafanikio makubwa ya utoaji wa chanjo mbalimbali kwa zaidi ya asilimia 90 na kuvuka lengo la kimataifa la asilimia 80

“Kwa niaba ya Wizara ya afya napenda kuwaeleza kuwa,kupitia ushirikiano huu mwaka 2015 Tanzania ilifanikiwa kutomeza ugonjwa wa Polio ambao ulikuwa tishio kwa maisha ya Watoto chini ya miaka mitano” amesema Bw.Tayari.

Aidha,ameeleza kuwa Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya imeweka mpango mkakati wa miaka mitano kuanzia 2026 hadi 2030 wa utekelezaji kuboresha huduma za chanjo (National Immmunization Strategy),amesisitiza mpango huo unalenga kujenga jamii imara ambayo kila mtoto atakingwa na magonjwa mbalimbali yanayozuilika kwa chanjo (vaccine preventable Diseaseses (VPDs).

Kwa upande wake Bw. Mario Jimenez meneja mwandamizi wa GAVI nchini Tanzania ameishukuru Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya kwa usimamizi bora wa utekelezaji wa shughuli za utoaji wa huduma za chanjo kipindi cha 2020 hadi 2025.amesema huduma hizo zimefanikwa kuwafikia Watoto wengi nchini na Watoto wa kike chini ya umri wa miaka 9 kwa ajili ya kuwakinga zidi ya saratani ya shingo ya kizazi