SERIKALI YASISITIZA UMUHIMU WA MATUMIZI NAMBA 199
Posted on: June 19th, 2025
Na WAF, Dar es Salaam
Kaimu Mkurugenzi wa huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya Dkt. Otilia Gowelle ametoa wito kwa watumishi kuendelea kufanya kazi kwa bidii huku akihimiza wananchi kutumia namba 199 bure ili kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali yahusuyo sekta ya afya nchini.
Dkt.Gowellen ametoa wito huo leo Juni 18,, 2025 wakati wa ziara ya kutembelea Kituo cha Elimu ya Afya kwa Umma cha Wizara ya Afya kilichopo Muhimbili Jijini Dar es Salaam na kuona kazi za uchapishaji na *Kituo cha Wizara ya Afya Cha kupokelea maoni na kujibu hoja za wananchi kuhusu masuala mbalimbali ya afya( *199 Afya Call )* kinavyofanya kazi.
"Nitoe wito kwa watumishi mfanye kazi kwa bidii, pia ni muhimu kwa kila mwananchi kujua umuhimu wa namba 199 bure ili kupata elimu na ufafanuzi kuhusu afya," amesema Dkt.Gowelle.
Katika ziara hiyo Dkt.Gowelle ameambatana na Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma Dkt. Ona Machangu.
Aidha, Dkt. Gowelle ametembelea Kituo Afya Bandari ya Dwarves na kujionea kinavyofanya kazi.