Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

PROF. MAKUBI AWATEMBELEA WAGONJWA TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD NA KUWAPA ZAWADI ZA SIKUKUU

Posted on: December 25th, 2022


Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi ametembelea wagonjwa katika Taasisi ya Saratani Ocean Road ili kuwajulia hali na kutoa misaada ya sikukuu kwa niaba ya familia yake.

Akizungumza leo Desemba 26, 2022 alipotembelea wagonjwa katika Taasisi ya Saratani Ocean Road, Prof. Makubi amesema, Serikali tayari imekwishaanza ujenzi wa vituo vingine katika katika Hospitali Kanda ya Rufaa Mbeya, KCMC Kilimanjaro, Bugando Mwanza na Benjamin Mkapa iliyopo Dodoma.

Sambamba na hilo Prof. Makubi ametoa zawadi mbalimbali pamoja na kunywa nao chai kama ishara ya kuwatia moyo na kuwatakia ahueni kwenye magonjwa yanayowasumbua.

Pamoja na hayo, Prof. Makubi amefanya ibada fupi ya kuwaombea baraka ya uponyaji wa haraka toka kwa Mwenyezi Mungu ili warejee katika hali yao ya kawaida na kuchangia ujenzi wa taifa.

Aidha, Prof. Makubi amewataarifu kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anafahamu changamoto za wagonjwa wa Saratani nchini hivyo anaendelea kusimamia maboresho katika Sekta ya Afya katika kutoa elimu kwa jamii, kubaini mapema, kutibu na kuimarisha Tiba Shufaa Kwa wagonjwa wa Saratani nchini Tanzania.

Baadhi ya wagonjwa waliolazwa waliopo kwenye wodi wamemshukuru Prof. Makubi aliyeambatana na familia yake na pia Mkurugenzi wa Huduma za Tiba, Prof. Paschal Ruggajo kwa kuungana nao kwenye chai ikiwa ni ishara ya kuwajali.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dkt. Julius Mwaiselage amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kufanya maboresho katika taasisi hiyo ikiwemo kujenga majengo na kufunga mashine kisasa za Cyclotron, PET/CT Scan, MRI, na ICU ili kuwahudumia wananchi wa hali zote.

Aidha, Dkt. Mwaisalage amesema, dawa zote za tiba Saratani zinapatikana kwa asilimia 98 na kushukuru Serikali kupeleka fedha MSD ili kununua dawa hizo hali iliyosaidia kupunguza hadha wagonjwa hasa wasio na uwezo wa kununua dawa hizo.

Akizungumzia maandalizi ya kufungua kitengo cha upasuaji (surgical oncology) amesema, maandalizi yanaendelea vizuri