Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

MPANGO WA WAHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII WABADILISHA MTAZAMO WA WANACHI LINDI

Posted on: June 16th, 2025

Imeelezwa kuwa Mpango wa Mafunzo ya Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii (CHW) umebadilisha mtazamo wa wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi baada ya wazazi kuwaruhusu vijana wao kuhudhiria mafunzo na kuhitimu mafunzo hayo.


Muuguzi wa zahanati ya Komolo katika Manispaa hiyo Bw. Leo Peter Manyanyi amesema wananchi wa maeneo hayo walikuwa hawatilii maanani masuala ya elimu lakini baada ya kuhamasishwa kuhusu mpango huu waliwaruhusu vijana wao waliochaguliwa kupata mafunzo na kuhitimu vyema.


" Hapa kijijini tuna vijana 12 waliohitimu mafunzo ya miezi sita yaliyoanza Oktoba, 2024 na kuhitimishwa Aprili 2024 , " amesema Bw. Manyanyi.


Omary Ibrahim ambaye ni miongoni mwa vijana 12 wa kijiji cha Komolo  aliyehitimu mafunzo ameishukuru Serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa mpango wa mafunzo ambao kwao ilikuwa kama ndoto lakini imetimia na imebadilisha maisha yao.


Kijana Ibrahim amesema tayari wamekwishapatiwa baiskeli kama  kitendea kazi.



Mpango mafunzo kwa wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii ulizinduliwa Rasmi na Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango tarehe 31 Januari, 2024 ambao utawezesha kuwapatia mafunzo wahudumu  waAfya Ngazi ya Jamii 137,294. Watakaotekeleza  Mpango Jumuishi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii.