KITABU SAFARI UPANDIKIZAJI MOYO, MAPINDUZI SEKTA YA AFYA NCHINI
Posted on: June 12th, 2026Na Zakayo Mosha WAF-Dar es salaam
Waziri wa afya mheshimiwa Mohamed Mchengerwa amezindua bodi ya wadhamini ya Taasisi ya moyo Jakaya kikwete (JKCI) ikiwa ni hatua ya kuendelea kuimarisha utoaji wa huduma za moyo nchini na kupunguza gharama za wagonjwa kutubiwa nje ya nchi.
Akizindua bodi hiyo leo Juni 12,2026 jijini Dar es salaam Waziri wa afya mhe.Mohamed mchengerwa amemtaka mwenyekiti wa bodi na wajumbe wake kufanya wajibu walioaminiwa kwa uadilifu na weledi ili kufikia malengo ya Serikali ya awamu ya Sita.
"Ndugu zangu wajumbe naomba mfanye kazi za kutafuta wadau kwa kushirikiana na mkurugenzi wenu Dkt.Kisenge na kama na kibali cha kufanya kazi hiyo ndiyo nimeshakitoa kwa tamko hili,pia nawataka bodi zote nchini pamoja na wataalam tutoke kutafuta wadau wa kuunga mkono serikali katika kuboresha sekta ya afya" amesema na kuongeza Waziri Mchengerwa.
Aidha,amesema Taasisi ya moyo JKCI imeendelea kuwa mfano bora na wakuigwa hapa Tanzania,nawata wataalam wetu kujiokeza katika vyombo vya habari na kuwaeleza watanzania mafanikio makubwa yaliyopatikana katika taasisi yenu kwani wengi hawajui.
Akizungumza baada ya uzinduzi wa bodi hiyo,Dkt.Hassan Mshindo Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini ya JKCI amesema wamepokea maelekezo yote yaliyotolewa na Waziri wa afya tayari kwa utekelezaji.
"Tutafanya kazi zetu na wajibu tuliopewa kama dhamana kwa watanzania kwa lengo la kuhakikisha JKCI inakuwa taasisi bora Afrika mashariki na kati na afrika kwa ujumla" amesema Dkt.Mshinda
Akihitinisha Dkt.Mshinda ametoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kumteua mtu kazi waziri wa afya Mohamed mchengerwa ambaye amekuwa kiongozi wa vitendo na hivyo kujenga matumaini mapya kwa watanzania kuendelea kupata huduma bora za afya na zenye utu na staha.