HUDUMA JUMUISHI ZA MAMA NA MTOTO MCHANGA KUIMARISHWA, GEITA, KATAVI NA KIGOMA
Posted on: February 13th, 2026Na WAF, Geita
Utambulisho wa mradi wa Mama na mtoto Mjamzito unalenga kuboresha upatikanaji na ubora wa huduma kwa mama wajawazito, wanaojifungua na watoto wachanga.
Hayo yamebainishwa leo Februari 12, 2026, na Mkuu wa mkoa wa Geita, Mhe. Martin Shigela, wakati wa uzinduzi wa mradi wa mjamzito na mtoto salama mkoani humo.
Mhe. Shigela amesema lengo la mradi ni kuimarisha huduma za kliniki ya wajawazito, huduma jumuishi za dharura kwa mama na mtoto, tiba kinga ya kutokwa damu baada ya kujifungua, pamoja na huduma za watoto wachanga.
“Mkoa wa Geita umeendelea kupiga hatua na kupunguza vifo vya mama na wajawazito kupitia ujenzi wa uwezo wa wataalamu wa afya na ongezeko la vituo vya afya kutoka 189 hadi 387 nchini, hatua inayodhihirisha dhamira ya Serikali chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kupunguza vifo vya mama na mtoto,” amesema Mhe. Shigela.
Kwa upande wake wa Wizara ya Afya, Joachim Masunga, amesema Serikali imeweka nia ya dhati ya kuhakikisha inaendelea kuweka mikakati madhubuti ya kupunguza idadi ya vifo vinavyotokana na uzazi kwa kushirikisha wadau mbalimbali ili kufanikisha utekelezaji wa mradi huo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Thamini Uhai, Banzi Msumi, alishukuru Serikali kupitia Wizara ya Afya na ofisi ya waziri mkuu TAMISEMI kwa ushirikiano walioutoa kwa wadau.
Aidha, amesema mradi huu ni wa Serikali, na Thamini Uhai itahakikisha utekelezaji wake unachangia kuimarisha ubora wa huduma za mama na mtoto katika mikoa ya Geita, Katavi, na Kigoma.
Akizungumza kwenye hafla hiyo Mkurugenzi wa Miradi kutoka Shirika la Thamini Uhai, Dkt. Sunday Dominico, amesema mradi huu wa miaka mitano utafanikiwa kutekelezwa katika mikoa ya Kigoma, Katavi, na Geita.
Dkt. Sunday ameongeza kuwa mradi huu unafadhiliwa na Bloomberg Philanthropies na Gates Foundation, wadau wa maendeleo wanaoshirikiana na Serikali katika sekta ya afya.
Amesema wadau hao watashirikiana kwa karibu katika utekelezaji wa mradi ili kuchangia juhudi za serikali za kuhakikisha malengo ya kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua yanafikiwa, kuelekea