Wizara Ya Afya

HOSPITALI ZINAZOTOA HUDUMA ZA NEUROSURGERY NCHINI ZAONGEZEKA

Posted on: April 20th, 2026

Na Hassan Kimweri, WAF - Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema idadi ya hospitali zinazotoa huduma za neurosurgery zimeongezeka kutoka hospitali mbili zilizokuwepo miaka ya nyuma hadi kufikia hospitali saba Aprili 2026 ambapo ongezeko hilo linaonyesha uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya nchini.

Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema hayo leo Aprili 16, 2026 katika Mkutano wa pili wa kimataifa wa shirikisho la jumuiya ya madaktari wa upasuaji wa ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

"Hatua hii inaonesha mabadiliko ya Tanzania kutoka kuwa na uwezo mdogo wa huduma za upasuaji wa ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu (neurosurgery) kwenda katika mfumo imara, endelevu na unaojitegemea wa huduma bora za kibingwa," amesema Rais Samia

Amefafanua kuwa uwekezaji huo umechangia kuongezeka kwa idadi ya upasuaji unaofanyika nchini pamoja na kuboresha matokeo ya matibabu kwa wagonjwa katika hospitali mbalimbali.

Aidha, Rais Samia amesema Serikali imefanikiwa kuimarisha nguvu kazi ya wataalamu wa upasuaji, ambapo idadi ya madaktari bingwa imeongezeka kutoka elfu 1,038 mwaka 2020 hadi kufikia elfu 1,338 Aprili 2026, sawa na ongezeko la wataalamu 542 katika kipindi hicho.

"Idadi ya wataalamu wa neurosurgery nchini imeongezeka mara tatu kutoka 12 hadi kufikia 37, hatua inayosaidia kuokoa maisha ya wananchi wengi zaidi, hususan wanawake na watoto wanaohitaji huduma za dharura za upasuaji wa ubongo na uti wa mgongo," amesema Rais Samia

Pia, Rais Samia amewahakikishi wananchi kuwa Serikali inahimiza matumizi ya ujuzi wa kitaalamu na ubobezi, huku ikiendelea kuongeza fursa kwa wanawake katika sayansi, teknolojia na fani za kibingwa ili kuhakikisha usawa na maendeleo jumuishi katika sekta ya afya.

"Mafanikio haya yametokana na mipango ya makusudi ya Serikali, ikiwemo Mpango wa Ufadhili wa Samia Scholarship and Fellowship Programme, pamoja na ushirikiano wa kimataifa kupitia taasisi kama CECTA, WFN